WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ina mkakati wa kufanya Majiji
yote nchini yawe na barabara za viwango vya kimataifa na zinazopitika
kwa urahisi.
“Tumeanza
kujenga barabara za kisasa katika jiji la Arusha ambalo ni jiji la
utalii, tutakwenda Mwanza na Dar es Salaam kwa kujenga barabara zenye
njia za juu (flyovers) zikiwemo za magari na za waenda kwa miguu,” amesema.
Ametoa
kauli hiyo Alhamisi, Mei 4, 2017 wakati akizumngumza na wananchi wa
Tengeru, wilayani Arumeru, mkoani Arusha mara baada ya kukagua barabara
ya Sakina- Tengeru yenye urefu wa km. 14.1 ambayo itakuwa na njia nne za
magari.
“Nimekuja
kukagua ujenzi wa barabara hii ya Sakina hadi Tengeru lakini mkandarasi
akimaliza anajenga barabara nyingine ya kilometa 42.1 na hivyo hapa
Arusha tutakuwa na kilometa 56.5 za awamu ya kwanza,” alisema.
Alisema
maboresho ya barabara za Jiji la Arusha yanafanyika ili kuwezesha
wafanyabiashara kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi na viwanda
vitakapoanza kujengwa, itakuwa hawana shida ya mawasiliano.
Akizungumzia
tatizo la uhaba wa ardhi aambalo lililibuliwa na mbunge wa Arumeru
Mashariki, Bw. Joshua Nassari, Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa Mkoa wa
Arusha, Bw, Mrisho Gambo aendelee na zoezi la kuuzungukia mkoa wake ili
kubaini maeneo yenye matatizo sugu.
Mapema,
akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara hiyo kwa Waziri Mkuu, Kaimu Meneja
wa TANROADS Mkoa wa Arusha, Eng. Mgeni Mwanga alisema ujenzi wa
barabara hiyo ambao ulianza Juni 2015, unatarajia kukamilika Juni 2018.
“Ujenzi
wa barara ya Sakina –Tengeru ni wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa
barabara yenye urefu wa km. 230 ya kutoka Arusha –Holili- Taveta –Voi
ambayo ujenzi wake unatarajiwa kugharimu sh. bilioni 139.34. Ujenzi huo
unagharimiwa na Serikali ya Tanzania pamoja na Benki ya Maendeleo ya
Afrika (AfDB).
Sambamba
na barabara hiyo, Eng. Mwanga alisema mkandarasi wa barabara hiyo
ataanza kujenga barabara nyingine ya km. 42.1 inayoanzaia Usa River hadi
Kisongo kwa kiwango cha lami ambayo itakuwa na madaraja saba wakati ile
ya Sakina hadi Tengeru ina madaraja makubwa mawili.
Naye
mbunge wa Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari alisems uhaba wa ardhi
bado ni tatizo kubwa kwenye wilaya hiyo kiasi kwamba hawana hata eneo la
kujenga shule au zahanati.
“Maeneo
yote yameuzwa na wenyeviti wa vijiji na madiwani, hivi sasa ukitaka
kujenga shule au zahanati hakuna eneo hata moja. Mheshimiwa Waziri Mkuu
tunaomba utusaidie kufuatilia suala hilo licha ya kuwa Waziri wa Ardhi
na Maendeleo ya Makazi alishakuja na kuelezwa hali halisi ilivyo,” alisema.
www.shudate.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment