Nchi saba miongoni mwao ni za kiafrika. Aidha mtandao huo haujaijumuisha nchi ya Uganda katika orodha hiyo, ingawa majeshi ya nchi hiyo yamekuwa mstari wa mbele katika kuimarisha majeshi ya kulinda amani barani Afrika, na inasemwa kuwa ni moja ya nchi yenye majeshi yaliyofunzwa vizuri barani humu. Tuangalie hizo nchi saba na kwa nini zinahesabiwa kuwa zina majeshi yenye nguvu barani Afrika.
Misri
Nchi ya Misri ni nchi ya kwanza ya kiafrika kuingia katika orodha hii ikishika nafasi ya 14. Majeshi ya Misri yamegawika katika makundi manne: Jeshi la ulinzi, jeshi la majini, jeshi la angani na kitengo cha ulinzi wa anga. Kwa mujibu wa Global Firepower, Misri ina zaidi ya ndege za kijeshi 800 na helikopta 200. Pia jeshi la majini la Misri limearifiwa kuwa lina meli ndogo 2 za kivita ambazo ni maalumu kwa kusindikiza na manuari 4 pamoja na vyombo vingine vya majini kuhakikisha ulinzi.
Moja ya sababu iliyofanya nchi ya Misri kuwa katika nafasi ya juu ni kutokana na msaada kutoka majeshi ya kimataifa – katika namna yoyote msaada huu huja katika mfumo wa vifaa vya kijeshi. Nchi ya Marekani inaisadia Misri msaada wa kijeshi kila mwaka kuhakikisha usalama katika bara hili la Afrika; inaarifiwa kuwa nchi hiyo imeisaidia Misri jumla ya Dola 1.39 billion mwaka huu wa 2013. Misri imekuwa ikisaidia pia nchi mbalimbali barani humu, zikisaidia kufundisha majeshi yao; ingawa lengo kubwa la majeshi ya Misri ni mashariki ya kati kuliko Africa. Kwa mujibu wa taarifa pia ni kuwa, majeshi ya Misri yanamiliki uchumi mkubwa, hadi kufikia 40%.
Ethiopia
Jeshi la Ethiopia linaundwa na Jeshi la ulinzi na jeshi la anga na inashika namba mbili kwa kuwa na jeshi lenye nguvu barani Afrika kwa sababu mbili; idadi kubwa ya watu na kuwa huru kwa kipindi kirefu. Mapema mwaka huu, iliripotiwa kuwa jeshi la Ethiopia limeendeleza ndege yao ya kwanza isiyo na rubani; huku teknolojia yake ikihusishwa na nchi ya Marekani.
Nchi hii hujihusisha na uhifadhi wa amani wa kimataifa kuhakikisha inasuluhisha migogoro barani Afrika. Mwaka 2012 nchi ya Ethiopia iliripotiwa kuwa na wanajeshi wapatao 150 000 katika jeshi la ardhini na zaidi ya wanajeshi 3000 wa jeshi la anga. Global Firepower inaripoti kuwa nchi hii ina zaidi ya vifaru 300, ndege za kivita 147 na helkopta 68.
Afrika Kusini
Jeshi la ulinzi la taifa la Afrika Kusini linajumuisha jeshi la ulinzi, jeshi la majini na jeshi la anga, na jeshi maalumu la huduma za afya. Kwa mujibu wa Global Firepower ghala la silaha katika nchi hii linahifadhi vifaru 250, rocket 240, ndege za kivita 235 na manuari 3. Wakati nchi hii ya Afrika Kusini ikitajwa kuwa na jeshi dogo kwa idadi ya wanajeshi, lakini linachukuliwa ndiyo jeshi lilioendelea katika masuala ya teknolojia.
Kabla ya kufikia ukomo wa siasa za ubaguzi wa rangi nchini humo, nchi hiyo ilikuwa tayari imeendelea katika silaha za nyuklia, na licha ya kuziharibu silaha hizo, bado kuna kiwanda ama ustawi wa silaha nchini humo. Sasa nchi hii inaanza kuchukua hatua kadhaa kwa ajili amani ya bara la Afrika, lakini kwa tukio la hivi karibuni lililotokea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati limeonesha udhaifu wa jeshi hilo.
Nigeria
Jeshi la nchu ya Nigeria linaundwa na wanajeshi wapatao 500 000, waliogawanyika baina ya jeshi la ulinzi, jeshi la majini na jeshi la anga. Jeshi hili nalo limekuwa mstari wa mbele katika kuunganisha nguvu ili kulinda amani ya kimataifa barani Afrika. Kwa mujibu wa Global Firepower, nchi ya Nigeria inamiliki vifaru 363, ndege za kivita 294 na helkopta 84. Jeshi la Nigeria kwa ujumla wake limekuwa makini zaidi katika upande wa kaskazini mwa nchi hiyo.
Pia jeshi hili linashutumiwa kwa kutumia mabavu mengi katika kushughulikia masuala ya raia na mgogoro wao na kundi la Boko Haram. Jeshi la majini pia lina meli za kivita 4. Uimara huu wa jeshi la Nigeria ni matokeo asili ya siasa za Nigeria tangu kupata uhuru wake. Kuna mapinduzi ya kijeshi 10 nchini Nigeria kati ya mwaka 1966 na 1999 huku kukiwa na vita vya ndani kati ya mwaka 1967 na 1970. Bajeti ya jeshi kwa mwaka ni dola 3.7 billion.
Algeria
Jeshi la Algeria linajulikana pia kama Jeshi la taifa la Watu. Jeshi hili limeimarika katika sehemu zote yaani kwa idadi ya wanajeshi ambapo lina zaidi ya wanajeshi 120 000 na wameimarika katika vifaa huku wakiungwa mkono na nchi za Urusi na China. Jeshi hilo linajengwa na jeshi la ulinzi, jeshi la maji na jeshi la anga. Jeshi la Algeria linamiliki vifaru vipatavyo 1050 kwa mujibu wa Global Firepower. Pia wanaripotiwa kumiliki roketi 148, ndege za kivita 409, helkopta 136, meli 3 za kivita na manuari 3.
Inaaminika kuwa jeshi la Algeria linajihusisha na siasa za ndani; hii inaweza kuwa ni matokeo ya kutokuwa na jambo la kufanya kwani hawajawahi kujihusisha na masuala ya utunzaji wa amani ama kushughulikia migongano ya kimataifa tangu mwaka 1976. Mapema Januari mwaka huu, majeshi ya Algeria yalihusika katika operation ya kuwaachia huru mateka katika kiwanda cha Sahara gas plant. Wakati watekaji 32 wakiripotiwa kuuawa, lakini mateka ndiyo waliuawa wengi kwani waliuawa mateka 48.
Kenya
Majeshi ya ulinzi ya Kenya, kama ambavyo yanatambulika katika taifa hilo la Afrika Mashariki, linajumuisha jeshi la ulinzi, jeshi la maji na jeshi la anga. Likiwa na wanajeshi 24 120 tu, ni moja kati jeshi dogo Barani Afrika; ingawa mbinu zake kitaifa hulifanya jeshi hilo kuwa kali zaidi tangu kuanzishwa kwake. Linasaidiwa na nchi ya Marekani na lina bajeti inayofikia dola 800 million kwa mwaka.
Kwa mujibu wa Global Firepower, jeshi la Kenya lina vifaru 186, roketi 12, ndege za kivita 148 na helkopta 78. Jeshi la Kenya limekuwa likijihusisha na mipango mbalimbali ya Umoja wa Mataifa ya utunzaji wa amani barani Afrika na Ulaya. Pia limefanya kazi pamoja na jeshi la Somalia kwa ajili ya kupambana na kundi la Al-Shabaab na limejiunga na Umoja wa Majeshi ya Afrika nchini Somalia (AMISOM).
Libya
Kihistoria nchi ya Libya lilikuwa na jeshi kubwa barani Afrika, lakini kufuatia mapinduzi ya nchi hiyo mwaka 2011 jeshi hilo lilivunjwa na kuanzishwa Jeshi la Taifa la Libya. Kwa sasa jeshi la Libya lina wanajeshi kati ya 35 000 na 40 000.
Ghala ya silaha ya jeshi hili limerithiwa kutoka jeshi la awali lililojulikana kama Arab Jamahiriya. Jeshi hilo sasa linaundwa na jeshi la ardhini, jeshi la maji na jeshi la anga. Kwa mujibu wa Global Firepower jeshi la Libya linamiliki vifaru 500, roketi 800, ndege za kivita 621, meli kubwa ya kivita na ndogo.
shudate blog
0 comments:
Post a Comment