UNIA haiishi vituko na mara zote kumekuwa kunaibuka kwa vituko
mbalimbali ambavyo kwa ujumla wake vinasaidia katika kuifanya Dunia kuwa
eneo la watu kuishi na kufurahi.
Makala haya ya kimataifa wiki hii yameangazia hoteli ya kifahari
wanamozuiliwa wana wa wafalme Saudi Arabia Ritz – Carlton ni jina la
moja ya hoteli za kifahari zilizo maarufu kote duniani.
Marais, Mawaziri Wakuu na wafalme wamekaribishwa katika hoteli hizo
ya Ritz-Carlton mara kadhaa. Lakini kwa mujibu wa ripoti kadhaa, hoteli
hizo zilizo katika mji mkuu wa Saudi Arabia wa Riyadh yamekuwa gereza.
Watu kadhaa mashuhuri nchini Saudi Arabia sasa wanaripotiwa kuwekwa
kizuizini katika hoteli hiyo inayotumika pia kufikia wageni mashuhuri wa
serikali huku hoteli hiyo ikitajwa kuwa gereza la kifahari zaidi
duniani.
Wana wa wafalme 11, mawaziri wanne na watu wengine kadhaa wamekamatwa
katika kile mamlaka za Saudi Arabia zinasema kuwa ni kampeni ya
kupambana na ufisadi nchini humo. Bilionea maarufu duniani humo, Prince
Alwaleed bin Talal anaripotiwa kuwa miongoni mwa wale waliokamatwa na
kushikiliwa katika gereza hilo la aina yake.
Mtandao wa gazeti la The New York Times ulichapisha kanda ya video
iliyoonesha matumizi hayo mengine mapya ya Hoteli ya Ritz-Carlton
Riyadh. Katika video hizo walinzi wanaonekana wamelala kwenye mikeka
katika chumba kimoja cha hoteli, watu wenye sare pia nao wanaonekana
huku bunduki zikionekana zikiegeshwa kwenye ukuta.
Gazeti la Guardian liliripoti kuwa wageni waliombwa siku ya Jumatano
jioni wakusanyike sehemu moja na mizigo yao, kabla ya kusafirishwa
kwenda kwa hoteli zingine mjini Riyadh ili kuifanya hoteli hiyo kubakia
na jukumu moja la kuwahifadhi wafungwa.
The Guardian imemnukuu ofisa mmoja wa Saudi Arabia akisema kuwa
mamlaka hazingeweza kuwaweka watu hao gerezani na hilo lilikuwa suluhu
bora. Jitihada za kulipia vyumba katika hoteli hiyo siku ya Jumanne
hazikuzaa matunda.
Hatua hiyo imekuja katika wakati ambao nchi hiyo imekuwa inachukua
hatua mbalimbali za kubadili mifumo ya kimaisha. Hivi karibuni Saudi
Arabia ilitangaza kuanza kuwaruhusu wanawake kuhudhuria michezo katika
viwanja vya michezo kwa mara ya kwanza kuanzia mwaka ujao.
Sasa familia zitaweza kuingia kwenye viwanja vitatu vya michezo vya -
Riyadh, Jeddah na Dammam. Ni hatua nyingine ya kuwapa wanawake wa Saudi
Arabia uhuru zaidi, ambao kawaida hukumbwa na ubaguzi wa kijinsia na
baada ya kuondolewa marufuku ya kuendesha magari.
Mfalme Mohammed bin Salman yuko katika harakati kubwa kuifanya Saudi
Arabia kuwa nchi ya kisasa na kuboresha uchumi. Mabadiliko hayo
yanaambatana na mipango mikubwa ya mabadiliko yaliyotangazwa na mfalme
huyo wa umri wa miaka 32 kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi kwa
taifa hilo linalotegemea mafuta, yanayojulikana kama maoni ya mwaka
2030.
Mwaka jana amri ya kifalme ilisema kuwa wanawake wanaweza kuendesha
magari kwa mara ya kwanza kuanzia mwezi Juni mwaka huu. Warsha
zinafanywa na sinema zinatarajiwa kurejeshwa tena.
Siku ya Jumatano Prince Mohammed alisema kurejeshwa kwa Uislamu wa
wastani ni kiungo muhimu cha kuifanya nchi kuwa ya kisasa. Alisema kuwa
asilimia 70 ya watu nchini Saudi Arabia wana umri wa chini ya miaka 30
na alisema kuwa wanahitaji maisha ambayo yanastahili dini.
Lakini wadadisi wanasema mipango haitakosa pingamizi. Wanawake nchini
Saudi Arabia bado ni lazima wafuate mitindo ya mavazi na wasiwe na
mahusiano na wanaume wasiostahili
0 comments:
Post a Comment