WAKATI umefi ka kwa mamlaka husika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo
mikoani ya Ubungo jijini Dar es Salaam kuwoandoa wapiga debe kutokana na
kero wanayosababisha kwa wasafi ri au abiria.
Wasafiri wanaoelekea mikoani wanajikuta katika usumbufu mkubwa kutoka
kwa wapiga debe hao ikiwemo kuulizwa maswali ya wapi wanakwenda lakini
pia kuvutwa huku na huku wakiwalazimishwa waseme wapi wanaenda.
Katika hali ya kawaida ni vigumu kuamini kwamba wasafiri hawajui
wanakokwenda na hivyo wanahitaji msaada wa wapiga debe hao. Kila mtu
anasafiri kwa mipango yake na hivyo anajua wapi anakokwenda na anajua
basi atakalosafiri nalo.
Mbali na usumbufu wa kuulizwa maswali ya ‘unakwenda wapi?’ pamoja na
kuvutwa huku na huku, lakini pia usalama wa mizigo ya wasafiri unakuwa
mdogo kutokana na hali hiyo.
Kwa kuwa imewahi kusikika mara kadhaa kuwa serikali inataka kuanzisha
utaratibu kwa wenye mabasi kutoa tiketi za kielektroniki, naamini mfumo
huu utakuwa suluhu kwa usumbufu ambao wasafiri wanaupata nyakati za
alfajiri wanapofika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo.
Mfumo wa tiketi wa kielektroniki ukianzishwa, utawasaidia wasafiri
kufika kwenye ofisi za basi husika kukata tiketi, na kwa utasaidia huo,
utaondoa kero ya wapiga debe ndani ya stendi hiyo.
Aidha, watoa huduma wa mabasi hayo kama watapewa mafunzo ya namna ya
kuwahudumia abiria wanaotaka kusafiri na mabasi yao, itasaidia kufanya
huduma za usafiri kwenye stendi ya Ubungo na kwingineko kuwa za kisasa
na za kistaarabu.
Kwa mfumo uliopo sasa ni rahisi pia kwa wasafiri kutapeliwa kutokana
na kila mtu kuwa na kitabu cha kukatishia tiketi. Utakuta basi moja lina
wapiga debe zaidi ya sita na wakatisha tiketi zaidi ya watatu, hivyo
inakuwa vigumu kuamini kama anayekuhudumia ndiye mhudumu sahihi.
Wito wangu ni kwa mamlaka husika kujipanga na kuondoa kero hii.
Usafiri wetu unapaswa kuwa wa kisasa katika huduma kuanzia utoaji wa
tiketi, huduma wanazopata abiria wakati wote wa safari, lugha za
wahudumu kwa abiria na mwendo ambao ni salama kwa abiria hili
linalofanyika Ubungo ni la ujima zaidi.
Kwa kuwa tunahitaji ustaarabu na utaratibu mzuri katika huduma za usafiri nchini, zoezi la kuwaondoa wapiga debe lifanyike
0 comments:
Post a Comment