Sunday, November 12, 2017

Wapiga debe Stendi Kuu Ubungo sasa basi

Image result for ubungo       Image result for ubungo      



















WAKATI umefi ka kwa mamlaka husika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani ya Ubungo jijini Dar es Salaam kuwoandoa wapiga debe kutokana na kero wanayosababisha kwa wasafi ri au abiria.
Wasafiri wanaoelekea mikoani wanajikuta katika usumbufu mkubwa kutoka kwa wapiga debe hao ikiwemo kuulizwa maswali ya wapi wanakwenda lakini pia kuvutwa huku na huku wakiwalazimishwa waseme wapi wanaenda.
Katika hali ya kawaida ni vigumu kuamini kwamba wasafiri hawajui wanakokwenda na hivyo wanahitaji msaada wa wapiga debe hao. Kila mtu anasafiri kwa mipango yake na hivyo anajua wapi anakokwenda na anajua basi atakalosafiri nalo.
Mbali na usumbufu wa kuulizwa maswali ya ‘unakwenda wapi?’ pamoja na kuvutwa huku na huku, lakini pia usalama wa mizigo ya wasafiri unakuwa mdogo kutokana na hali hiyo.
Kwa kuwa imewahi kusikika mara kadhaa kuwa serikali inataka kuanzisha utaratibu kwa wenye mabasi kutoa tiketi za kielektroniki, naamini mfumo huu utakuwa suluhu kwa usumbufu ambao wasafiri wanaupata nyakati za alfajiri wanapofika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo.
Mfumo wa tiketi wa kielektroniki ukianzishwa, utawasaidia wasafiri kufika kwenye ofisi za basi husika kukata tiketi, na kwa utasaidia huo, utaondoa kero ya wapiga debe ndani ya stendi hiyo.
Aidha, watoa huduma wa mabasi hayo kama watapewa mafunzo ya namna ya kuwahudumia abiria wanaotaka kusafiri na mabasi yao, itasaidia kufanya huduma za usafiri kwenye stendi ya Ubungo na kwingineko kuwa za kisasa na za kistaarabu.
Kwa mfumo uliopo sasa ni rahisi pia kwa wasafiri kutapeliwa kutokana na kila mtu kuwa na kitabu cha kukatishia tiketi. Utakuta basi moja lina wapiga debe zaidi ya sita na wakatisha tiketi zaidi ya watatu, hivyo inakuwa vigumu kuamini kama anayekuhudumia ndiye mhudumu sahihi.
Wito wangu ni kwa mamlaka husika kujipanga na kuondoa kero hii. Usafiri wetu unapaswa kuwa wa kisasa katika huduma kuanzia utoaji wa tiketi, huduma wanazopata abiria wakati wote wa safari, lugha za wahudumu kwa abiria na mwendo ambao ni salama kwa abiria hili linalofanyika Ubungo ni la ujima zaidi.
Kwa kuwa tunahitaji ustaarabu na utaratibu mzuri katika huduma za usafiri nchini, zoezi la kuwaondoa wapiga debe lifanyike

Hoteli ya kifahari yageuzwa gereza



 UNIA haiishi vituko na mara zote kumekuwa kunaibuka kwa vituko mbalimbali ambavyo kwa ujumla wake vinasaidia katika kuifanya Dunia kuwa eneo la watu kuishi na kufurahi.
Makala haya ya kimataifa wiki hii yameangazia hoteli ya kifahari wanamozuiliwa wana wa wafalme Saudi Arabia Ritz – Carlton ni jina la moja ya hoteli za kifahari zilizo maarufu kote duniani.
Marais, Mawaziri Wakuu na wafalme wamekaribishwa katika hoteli hizo ya Ritz-Carlton mara kadhaa. Lakini kwa mujibu wa ripoti kadhaa, hoteli hizo zilizo katika mji mkuu wa Saudi Arabia wa Riyadh yamekuwa gereza.
Watu kadhaa mashuhuri nchini Saudi Arabia sasa wanaripotiwa kuwekwa kizuizini katika hoteli hiyo inayotumika pia kufikia wageni mashuhuri wa serikali huku hoteli hiyo ikitajwa kuwa gereza la kifahari zaidi duniani.
Wana wa wafalme 11, mawaziri wanne na watu wengine kadhaa wamekamatwa katika kile mamlaka za Saudi Arabia zinasema kuwa ni kampeni ya kupambana na ufisadi nchini humo. Bilionea maarufu duniani humo, Prince Alwaleed bin Talal anaripotiwa kuwa miongoni mwa wale waliokamatwa na kushikiliwa katika gereza hilo la aina yake.
Mtandao wa gazeti la The New York Times ulichapisha kanda ya video iliyoonesha matumizi hayo mengine mapya ya Hoteli ya Ritz-Carlton Riyadh. Katika video hizo walinzi wanaonekana wamelala kwenye mikeka katika chumba kimoja cha hoteli, watu wenye sare pia nao wanaonekana huku bunduki zikionekana zikiegeshwa kwenye ukuta.
Gazeti la Guardian liliripoti kuwa wageni waliombwa siku ya Jumatano jioni wakusanyike sehemu moja na mizigo yao, kabla ya kusafirishwa kwenda kwa hoteli zingine mjini Riyadh ili kuifanya hoteli hiyo kubakia na jukumu moja la kuwahifadhi wafungwa.
The Guardian imemnukuu ofisa mmoja wa Saudi Arabia akisema kuwa mamlaka hazingeweza kuwaweka watu hao gerezani na hilo lilikuwa suluhu bora. Jitihada za kulipia vyumba katika hoteli hiyo siku ya Jumanne hazikuzaa matunda.
Hatua hiyo imekuja katika wakati ambao nchi hiyo imekuwa inachukua hatua mbalimbali za kubadili mifumo ya kimaisha. Hivi karibuni Saudi Arabia ilitangaza kuanza kuwaruhusu wanawake kuhudhuria michezo katika viwanja vya michezo kwa mara ya kwanza kuanzia mwaka ujao.
Sasa familia zitaweza kuingia kwenye viwanja vitatu vya michezo vya - Riyadh, Jeddah na Dammam. Ni hatua nyingine ya kuwapa wanawake wa Saudi Arabia uhuru zaidi, ambao kawaida hukumbwa na ubaguzi wa kijinsia na baada ya kuondolewa marufuku ya kuendesha magari.
Mfalme Mohammed bin Salman yuko katika harakati kubwa kuifanya Saudi Arabia kuwa nchi ya kisasa na kuboresha uchumi. Mabadiliko hayo yanaambatana na mipango mikubwa ya mabadiliko yaliyotangazwa na mfalme huyo wa umri wa miaka 32 kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi kwa taifa hilo linalotegemea mafuta, yanayojulikana kama maoni ya mwaka 2030.
Mwaka jana amri ya kifalme ilisema kuwa wanawake wanaweza kuendesha magari kwa mara ya kwanza kuanzia mwezi Juni mwaka huu. Warsha zinafanywa na sinema zinatarajiwa kurejeshwa tena.
Siku ya Jumatano Prince Mohammed alisema kurejeshwa kwa Uislamu wa wastani ni kiungo muhimu cha kuifanya nchi kuwa ya kisasa. Alisema kuwa asilimia 70 ya watu nchini Saudi Arabia wana umri wa chini ya miaka 30 na alisema kuwa wanahitaji maisha ambayo yanastahili dini.
Lakini wadadisi wanasema mipango haitakosa pingamizi. Wanawake nchini Saudi Arabia bado ni lazima wafuate mitindo ya mavazi na wasiwe na mahusiano na wanaume wasiostahili

Wakulima Chamwino wanavyoweza kuepushwa na changamoto ya ukame




UMASIKINI unaochochewa na ukosefu wa mavuno kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi, umeendelea kuwatikisa wakulima katika vijiji vya Wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma.
Hivi karibuni, mwandishi wa makala haya alifika katika vijiji vya Chamwino, Buigiri, Chinagali II na Mwegamile katika Tarafa ya Chilonwa na kuzungumza na wakulima, wafugaji pamoja na wadau wengine wa kilimo.
Katika makala haya, anaeleza namna ambavyo utekelezaji madhubuti wa mipango na mikakati ya kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi, unavyoweza kupunguza kama si kukomesha umasikini unaochochewa na uzalishaji mdogo katika kilimo.
Uzalishaji mdogo umejidhihirisha zaidi katika msimu wa mwaka 2016/17 ambao Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino, Athumani Masasi anasema upo upungufu wa tani 4,949 za chakula.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, takribani hekta 83,208 za mazao ya chakula zililimwa na zikazalishwa tani 82,569 za chakula. Mahitaji halisi ya wilaya hiyo yalikuwa tani 87,518. Kulingana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, wilaya ina wastani wa watu 330,543 na wastani wa watu 4.5 kwa kaya.
Akielezea namna uzalishaji ulivyoshuka, mkulima katika kijiji cha Buigiri, Olivia Chinyemba anasema mwaka 2015 alilima ekari moja ya mtama na kuvuna gunia tatu; mwaka jana akapata gunia mbili. Mwaka huu amepata gunia moja la uwele na kwa upande wa mahindi, katika ekari moja amepata debe moja.
Kwa upande wake, mkazi wa Kijiji cha Chinangali, Michael Mbena, mwaka juzi alilima ekari moja ya mahindi akaambulia gunia nne na ekari moja ya uwele alikopata gunia tano. Mwaka 2016/2017 alilima shamba la ukubwa huo huo akapata gunia mbili na nusu na uwele akapata gunia tano.
Mwaka huu anasema hakupata chochote. Ofisa Mifugo wa Kata ya Buigiri, Stephano Adeline, ingawa hana takwimu rasmi za uzalishaji katika kilimo, anakiri mavuno yamekuwa yakishuka mwaka hadi mwaka kuanzia 2014. “Takwimu kamili sina ila naongea kulingana na ninachokiona.
Mwaka 2014 mavuno yalikuwa mazuri, hata mwaka 2015 mazao yalianza vizuri lakini ilipofika mwishoni , mvua ikakatika,” anasema Adeline akisisitiza kuwa msimu wa 2016/17 hali imekuwa mbaya zaidi.
Asilimia tano ya wakulima 40 waliozungumza na mwandishi wa makala haya kwa nyakati tofauti kutoka vijiji hivyo vya Chamwino, Buigiri, Chinangali II na Mwegamile, wanaamini hakuna namna ya kukabili njaa na umasikini endapo mvua zitaendelea kutotabirika.
“Sisi hatuna majibu, bali tunamwachia Mungu... Ofisa Kilimo utambanaje? Kwani yeye ana chakula? Mungu ndiye anayejua hili tatizo la ukame. Tunamwachia Mungu mipango yake,” anasema mkulima wa Chinangali II, Michael Mbena.
Lakini pia wakulima 14 sawa na asilimia 35 ya waliohojiwa wanasema wataalamu, hususani maofisa ugani ndiyo wanapaswa kuja na suluhisho la uzalishaji mdogo unaochangia umasikini.
Mathalani, Japhet Mdachi, ambaye ni mkulima katika Kijiji cha Buigiri, anasema, maofisa kilimo na mifugo wa vijiji na kata wasisubiri mikutano ya hadhara ndipo wawape ushauri wa kuhimili ukame. Kadhalika, wakulima 24 sawa na asilimia 60 wanasema serikali ndiyo yenye suluhisho wakimaanisha halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Wizara ya Kilimo na Rais.
Hata hivyo, wakulima wote walipohojiwa kama wanaelewa mipango, miongozo au mikakati ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi katika kilimo, walisema hawafahamu. Pia baadhi ya maofisa ugani, wanasema hawafahamu vizuri mipango hiyo, Ofisa Mifugo wa Kata ya Chamwino, David Msimbe anasema: “Mimi ninachokiona, mabadiliko ya tabianchi, nayaelewa kwa sababu nimesoma.
Lakini mpango mkakati wa kitaifa au wa kiwilaya, kwetu sisi tunakuwa hatufahamu vizuri. Hatujui wilaya imejipangaje. Tunatumia uzoefu tu wa kule chuoni ni namna gani ya kuwasaidia wakulima.”
Mpango wa Kilimo wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi wa mwaka 2014-2019 (ACRP) ni miongoni mwa mipango ambayo wakulima, maofisa ugani, halmashauri na wadau wengine wanapaswa waielewe na kuitekeleza.
ACRP umeainisha maeneo, mikakati na mbinu za kilimo kinachohimili mabadiliko chenye tija kama vile udhibiti wa maji katika ardhi ikiwamo kilimo cha umwagiliaji, uvunaji wa maji na kuyahifadhi na kilimo cha matuta.
Mbinu nyingine zinazoainishwa katika mpango huu ni kuhusu mbegu bora huku mpango ukisisitiza matumizi ya mbegu fupi zinazohimili ukame; uboreshaji wa taarifa za hali ya hewa na kuhakikisha zinawafikia wakulima.
Wapo wanaohimiza Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kuandaa kalenda mpya ya kilimo, kwani inasemekana yapo matukio ya wakulima kupishana na kipindi cha mvua kutokana na mabadiliko ya tabianchi.
Programu ya Kitaifa ya Kilimo Kinachohimili Mabadiliko ya Tabianchi ya mwaka 2015 ni mkakati mwingine wa serikali. Programu hii ni dira kwa sekta ya kilimo, ikilenga kuhimili mabadiliko ya tabia nchi na kuwa na usalama wa chakula kwa maendeleo ya uchumi yanayoendana na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.
Upo pia Mwongozo wa Kilimo Kinachohimili Mabadiliko ya Tabianchi uliozinduliwa Mei mwaka huu ambao maofisa mipango na maofisa ugani wamepewa nguvu ya kupanga na kuandaa bajeti kwa ajili ya maendeleo ya kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi katika jamii wanazozitumikia.
Maofisa ugani wanatakiwa kuhamasisha na kufundisha wakulima kutumia mbinu za kilimo zinazohimili mabadiliko ya tabianchi kama vile uvunaji na utunzaji wa maji ya mvua; umwagiliaji kwa njia ya matone; hifadhi ya udongo na maji pamoja na kilimo cha matuta.
Mwongozo unataja Bima ya Mazao kuwa ni mbinu nyingine ya kuwaepusha wakulima kuingia hasara na hatimaye umasikini kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Kuhusu bima ya mazao, Mratibu wa Bima ya Mazao katika Shirika la Bima la Taifa, Prosper Peter anasema lengo ni kumfidia mkulima ikiwa mazao yameharibiwa na mvua au ukame yakiwa shambani.
Hata hivyo, Prosper anasema shirika lake halijaingiza rasmi bima hii sokoni. Lakini anasema itakapoingia hivi karibuni, imejielekeza kwenye mazao ya biashara. Aidha anasema hakujawa na utaratibu maalumu wa kumsaidia mkulima mdogo asiye na uwezo wa kuchangia katika mfuko wa bima.
“Baadhi ya nchi za wenzetu kumekuwa na utaratibu wa serikali kuchangia gharama ya bima ya mazao lakini Tanzania hakujawa na utaratibu kama huo,” anasema Prosper. Ofisa Tathimini na Ufuatiliaji wa Taasisi ya Dodoma Network Environment (DONET), Emmanuel James katika kuelezea suluhisho la tatizo, anasisitiza halmashaui kuweka kipaumbele kwenye utekelezaji wa mbinu za uhifadhi wa ardhi na maji ikiwamo kuendesha kilimo cha umwagiliaji.
James anashauri mbinu hizo ziende sambamba na kuwapa wananchi njia nyingine za kujipatia kipato wasitegemee kilimo pekee. Anatoa mfano wa ufugaji wa nyuki kuwa ni shughuli isiyohitaji mvua nyingi inayoweza kufanyika wilayani Chamwino na wakulima wakajipatia kipato.
Shirika limekwishatoa mizinga 60 kwa vijiji vya Idifu (wilaya ya Chamwino) na Kikombo (Manispaa ya Dodoma) kila kimoja. Pia kijiji cha Mayamaya na Asanje vimepewa mizinga 38 kila kimoja lengo likiwa ni kuwezesha jamii kujipatia kipato.
Katika kuelezea suluhisho la tatizo, Mkurugenzi wa Shirika la Climate Action Network (CAN) linaloshughulika na masuala ya mabadiliko ya tabianchi, Sixbert Mwanga, anahimiza wakulima kupatiwa utabiri wa hali ya hewa ulio sahihi, unaojielekeza kwenye eneo mahususi.
Mwanga ambaye ni mtaalamu wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi, anasema: “Siyo mkulima apewe utabiri wa jumla. Mfano utabiri unaotaja kuwa mvua itanyesha katika Kanda ya Kati, au utabiri unaosema mvua itanyesha mkoa wa Dodoma, hautoshi.
Mkulima asaidiwe kutumia taarifa za hali ya hewa zilizo sahihi,” anasema Mwanga. Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga anataja suluhisho lingine la tatizo ni wakulima kuzingatia mwongozo wa uzalishaji mazao kulingana na kanda za kilimo za kiikolojia badala ya kung’ang’ania mazao yasiyostawi katika maeneo yao.
Afisa Tarafa ya Chilonwa, Mohammed Mfaki anasema katika msimu ujao, wamepanga atakayelima mahindi zaidi ya inavyoshauriwa, hawatasita kuyafyeka kwa lengo la kuwafanya wakulima watii ushauri wa kitaalamu. Anatoa mfano kuwa baadhi ya wakulima wameendelea kupanda mahindi ambayo hayastawi katika maeneo yao.
Kulingana na mwongozo huo, mazao ya kipaumbele ya chakula katika Wilaya ya Chamwino ni mtama na njugu mawe na ya biashara ni zabibu na ufuta. Mazao mengine yanayoweza kulimwa ni alizeti, karanga mpunga na viazi vitamu.
Mwongozo huo umezingatia ikolojia ya wilaya hii yenye mwinuko wa meta 500 -1,400, mvua milimita 400 – 800 na udongo mwekundu na kichanga. Mkuu wa Idara ya Mazingira katika Wizara ya Kilimo, Shakwaanande Natai anasisitiza kuwa suluhisho ni mipango, miongozo na mikakati ya kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi kuwafikia wakulima

Thursday, October 26, 2017

PEMBEJEO BORA ZINAVYOWEZA KUCHOCHEA KILIMO BORA

Image result for kilimo bora                Image result for kilimo bora
KILIMO ni sekta inayotegemewa kiuchumi na Watanzania zaidi ya asilimia 75, kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wa kitakwimu uliofanywa na mashirika tofauti ya ndani na kimataifa, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), kwa mujibu wa ripoti yake ya 2013, kilimo kinachangia asilimia 30 ya pato la ndani (GDP) na asilimia 64 ya pato linalotokana na mauzo nje ya nchi.
Kilimo ni sekta inatoa ajira mara 11 zaidi ya sekta nyingine za uzalishaji nchini, hivyo kuifanya kuwa na umuhimu wa pekee katika kukuza uchumi wa nchi na kustawisha maendeleo ya watu.
Ni kutokana na umuhimu huo, mwaka jana Baraza la Kilimo nchini (ACT) liliratibu utafiti uliojielekeza katika mifumo ya usimamizi kwa matumizi ya pembejeo za kilimo, mnyororo wa usambazaji na namna zinavyochochea uzalishaji kwa mkulima.
Utafiti huo uliofanywa na kampuni ya Match Maker Associates kwa niaba ya ACT, ulielekezwa katika mikoa yenye kanda zinazonufaika na mradi wa SAGCOT na Kaskazini mwa nchi.
Ofisa anayeshughulikia sera katika ACT, Laetitia William anasema utafiti huo ulifanyika kwenye wilaya tatu na kuzilenga pembejeo chache ambazo ni mbolea, mbegu na kemikali zinazotumika kwenye kilimo.
Wilaya hizo na mazao yaliyotumika katika utafiti huo kwenye mabano ni Mbozi na Babati (mahindi), Kilombero (mpunga), Babati (alizeti na maharage). Kwa mujibu wa ripoti ya Wizara ya Kilimo, mahitaji ya mbegu zilizoboreshwa nchini yanakadiriwa kuwa zaidi ya tani za ujazo 120,000 kwa mwaka wakati kiasi kinachosambazwa ni tani za ujazo 35,352 sawa na asilimia 59.
Hata hivyo, ripoti hiyo inaeleza kuwa matumizi ya mbegu hizo yapo kwa kiwango kidogo, ikikadiriwa kwamba asilimia 25 ya mazao yanayovunwa yanatokana na mbegu zilizoboreshwa wakati asilimia 75 ni kutoka kwenye mbegu za asili.
Hali hiyo inatokana na ukubwa wa bei inayotozwa kwa mbegu zilizoboreshwa, upatikanaji wake, miundombinu na mtandao duni katika usambazaji. Mtafiti John Alinanuswe kutoka Match Maker Associate Limited, anasema utafiti huo, pamoja na mambo mengine ulibaini kuwa kutokana na upatikanaji fedha usiokuwa wa uhakika kwa Taasisi ya Uthibitisho Rasmi Mbegu (TOSCI), wakati mwingine unasababisha kuchelewa kwa utekelezaji wa majukumu inayojipangia hususani kwenye ofisi zake zilizopo Arusha, Mwanza, Mtwara, Njombe na Morogoro.
Hali hiyo, kwa mujibu wa taarifa ya utafiti, imechangia pia sehemu ya ziara za ukaguzi wa TOSCI kukasimiwa kwa maofisa wa serikali ngazi ya wilaya. Alinanuswe anasema licha ya Kamati ya Taifa ya Mbegu (NSC) kuitisha mkutano wa wadau wa mbegu mara moja kwa mwaka, lengo likiwa ni kujadili masuala yanayohusiana na sekta hiyo, mahudhurio si ya kuridhisha kutokana na ushiriki kuwa suala la hiari.
Hata hivyo, ripoti hiyo inakosoa kwamba vikao hivyo vinaitishwa na kufanyika kitaifa wakati katika ngazi ya wilaya ufanisi wake ni mdogo na mara nyingi havifanyiki kutokana na sababu tofauti ikiwamo taasisi za wadau wa pembejeo za kilimo kutohudhuria.
Aidha, taarifa ya kitengo cha zana za kilimo katika Wizara ya Kilimo, inaonesha kuwa mahitaji ya mbolea yaliongezeka kutoka mita za ujazo 485,000 kwa msimu wa 2011/2011 kufikia 885,019 mwaka 2015/2016.
Mtafiti Alinanuswe anasema utafiti uliofanywa umebaini kuwa ubadilishanaji taarifa kati ya mamlaka zinazosimamia sekta ya kilimo nchini dhidi ya wadau wanaoshirikiana nao ni mdogo. “Katika majadiliano na mamlaka tofauti za usimamizi wa kilimo, hatukupata ushahidi wa kumbukumbu za pamoja za wadau wanaojihusisha na uingizaji na biashara ya pembejeo za kilimo,” anasema.
Hata hivyo, mwakilishi wa Tosci, Mtafiti Mwandamizi Doroth Ole Meiludi anasema hali hiyo imeboreshwa na kwamba miongoni mwa mamlaka hizo na hususani taasisi hiyo ya uthibitisho wa mbegu ina kumbukumbu hizo zinazosaidia kuleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.
Lakini Alinanuswe anasema ukosefu wa kumbukumbu unasababisha ugumu katika kuisimamia sekta ya kilimo, kuwatambua wanaoshiriki vitendo viovu dhidi ya pembejeo na kuwachukulia hatua zinazostahili.
Anasema matokeo hayo yanaonesha kuwa mamlaka za usimamizi zinakabiliwa na upungufu wa rasilimali watu na fedha, akizitaja kuwa ni nyenzo muhimu zinazochochea ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wakati.
Kuhusu mnyororo wa usambazaji pembejeo nchini, matokeo ya utafiti huo yanaonesha kuwapo kiwango duni cha uratibu wa pamoja wa shughuli za taasisi zinazoundwa na kampuni za uingizaji na biashara ya pembejeo.
Kampuni hizo zipo huru kujiunga na taasisi tofauti zilizoundwa ambazo ni pamoja na Chama cha Wafanyabiashara ya Mbegu (Tasta) na Chama cha Mawakala wa Mbegu (Tanada).
Alinanuswe anasema taasisi hizo zimebainika kupitia utafiti huo hazina uratibu wa pamoja na hakuna mfumo wa kuwezesha zikidhi sera na kanuni za mfumo wa usambazaji pembejeo nchini na kwamba hazijajiunda kusaidia shughuli za wasambazaji pembejeo kuwa na ufanisi.
Mtafiti huyo anasema stadi za utawala wa biashara kwa washiriki wengi wa pembejeo za kilimo hazipo kwa kiwango cha kuibua uwazi na ufanisi katika mfumo wa utoaji huduma husika.
Alinanuswe anasema ongezeko la matumizi sahihi ya pembejeo linaweza kuchangia kuongezeka uzalishaji na faida kwa wakulima. Utafiti unabaini kuwa sekta hiyo bado inakabiliwa na changamoto kadhaa zikiwamo ufinyu wa masoko, ubovu wa miundombinu, ukosefu wa taarifa sahihi, fedha na bima, hali inayoweza kufifisha ufanisi kwa wakulima, ikiwa hazitapatiwa ufumbuzi.
Wakati huo huo utafiti umebaini kiwango cha uwapo wa pembejeo bandia za kilimo kushuka kwa mwaka jana ikilinganishwa na ilivyokuwa mwaka 2012. Anasema watoa taarifa katika utafiti huo walieleza kuwa mbolea, mbegu na viuatilifu haziwaathiri kwa kiwango kinacholingana kama ilivyokuwa awali, akitoa mfano kada chache kama za watumishi katika halmashauri za wilaya na wakulima pekee, walizungumza uwapo wa mbolea bandia.
Akasema kada hizo pamoja wafanyakazi wa kampuni za mbegu walieleza kuwa takribani asilimia 20 ya mbegu zilizopo kwenye soko zina ubora hafifu unaoziweka katika kundi la pembejeo bandia.
Waliohojiwa katika utafiti huo, wamekaririwa wakieleza kuwa hali ya pembejeo bandia ni mbaya zaidi kwa upande wa viuatilifu. MAPENDEKEZO Utafiti huo unapendekeza, pamoja na mambo mengine, kuwapo mapitio yenye lengo la kuboresha mamlaka za usimamizi katika sekta ya kilimo, kuboresha uratibu miongoni mwa mamlaka hizo ili zifanye kazi zikilenga kuboresha huduma kwa mkulima na kumpunguzia gharama za uzalishaji.
Mapendekezo mengine ni kutangaza kwenye gazeti la serikali majina ya wakaguzi wa mbegu, mbolea na viuatilifu katika ngazi za wilaya na kuwajengea uwezo ili watimize wajibu wao kwa ufanisi.
Pia kufanikisha upatikanaji wa taarifa zinazohitajika katika kusajili, biashara na kuingiza pembejeo za kilimo. Kuongeza kiasi cha faini kwa wahusika wa pembejeo bandia na fidia kwa waathirika wa vitendo hivyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania (ACT), Janeth Bitegeko anasema mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti huo ni jukwaa muhimu hasa katika kipindi hiki ambacho kasi ya utendaji kazi wa serikali ni kubwa, hivyo kuwapo uwezekano wa upungufu kadhaa kufanyiwa kazi tangu kufanyika kwa utafiti huo.
Bitegeko anasema kilimo ni biashara inayochangia maendeleo ya nchi, ustawi na uboreshaji huduma za jamii kutokana na fedha zinazopatikana kupitia kodi mbalimbali zinazotozwa kwenye sekta hiyo.
Ni kutokana na hali hiyo, Bitegeko anasema baraza limejikita katika kujenga uwezo wa wakulima na wadau wengine wa kilimo kuhusiana na mnyororo wa thamani ya mazao hususani katika kulima, kuvuna, kuuza na masoko

Wednesday, October 25, 2017

2019 World Economic Forum of Young Global Leaders – Call for Nominations

 

The WEF Forum of Young Global Leaders has established a comprehensive selection process for identifying and selecting the most exceptional leaders. Every year, thousands of candidates from around the world are proposed and assessed according to rigorous selection criteria. Only the very best candidates are selected and all efforts are extended to create a truly representative body. Reflecting the diversity of stakeholders, the Young Global Leaders include leaders from politics, business, civil society, academia, and arts and culture across seven geographic regions.

Selection Criteria:
· To be eligible for the Young Global Leaders Class of 2019, the candidate must have been born on or after 1 January, 1980.
· He/she has a recognized record of extraordinary achievement and a proven track record of substantial leadership experience. Typically, this means 5-15 years of outstanding professional work experience and a clear indication of playing a substantial leadership role for the rest of his or her career.
· He/she has demonstrated a personal commitment to serve society at large through exceptional contributions and a deep ethical fiber, and has earned significant trust at both local and global levels.
· He/she has an impeccable record in the public eye and good standing in his/her community, as well as show great self-awareness and a desire for learning.
· Candidates from the business sector must be responsible for the full operation of a qualifying corporation or division and must hold one of the following titles: President, Chairman of the Board, Chief Executive Officer, Managing Director, Managing Partner or Publisher, or equivalent of any of the above. If the company is a Member or Partner of the World Economic Forum, the candidate requires the approval of the CEO or Chairman of the Board of the respective company.
· Companies, organizations and entities can only nominate one candidate from the qualifying company every two years.
· Kindly note that self-nominations are not accepted.
Nomination and Selection Timeline
· 31 May: Close of nomination period
· Summer: The World Economic Forum shortlists candidates for further review
· Fall: The shortlisted candidates are reviewed by Heidrick & Struggles, recognised as one of the world’s leading executive search and leadership consulting firms
· Winter: A Selection Committee reviews the top candidates and selects 100 to be honoured as Young Global Leaders
· January of subsequent year: The candidates are informed of their selection as Young Global Leaders*
· March of subsequent year: The press announcement for the new Class of Young Global Leaders is released
* Due to the large number of nominations received, the World Economic Forum only contacts successful candidates regarding their selection to the Forum of Young Global Leaders. However, some candidates may be contacted as part of the due diligence process. 

For more Information follow the link below..
 https://www.weforum.org/pages/nominate-a-young-global-leader

TAMASHA LA 19 LA DUNIA LA VIJANA NA WANAFUNZI NCHINI URUSI



 

Vijana 28 kutoka Tanzania waliwakilisha nchi yetu katia tamasha la 19 la dunia la vijana na wanafunzi lililofanyika Sochi Urusi. Ni tamasha la 19 la Dunia la vijana na wanafunzi, ambalo limefanyika Sochi Urusi, kwa ambapo zaidi ya vijana 20,000 kutoka mataifa zaidi ya 184 walikutana kujadili maendeleo ya dunia kwa sasa na wakati ujao, pia kila nchi ilionesha utamaduni wao ikiwepo Tanzania. Suala zima ilikuwa ni kukutanisha vijana na wanafunzi kutoka ulimwengu wote kutafakari njia mpya za kutatua changamoto katika nchi zao na ulimwenguni.
Pia kujifunza jinsi Urusi ilivyo endelea kiviwanda, teknolojia, uongozi, utamaduni na kutazama upya mambo ya uchumi, kujitawala na kujitegemea na sio kunyonywa na mabepari au kutegemea misaada sana ambayo imeleta migogoro hasa nchi zinazoendelea.
Kingine ni kuona jinsi umoja wa mataifa unafanya kazi kwa kusimamia maazimio pia na kujadili changamoto zake.
Katika malengo ya ulimwengu SDGs tumeona ya UN yapo 17 lakini ya WFYS2017 tumeongeza 18 ambalo ni Technology as a way of innovations and sustainable development to any country (Putin aliiongelea hii sana). Mmoja kati ya watanzania (Peter Mmbando) yeye aliweza kuongelea amani za maziwa makuu na matumizi ya artificial intelligence katika kumaliza migogoro lakini mazungumzo ni njia sahihi
Baada ya Tamasha kuisha vijana walipat furs yauweza kutembelea baadhiya maeneo ambayo ni yakitalii lakini kikubwa walichokiona au kutembelea ni kuona viwanja vitakavyotumika katika kombe la dunia hapo mwakani 2018



































Kijana Peter akiwa katika mja ya viwanja vitakavyochezewakombe la dunia hapo mwakani 2018



kijana peter akibadilishana mawazo na Dr. Walter Schwimmer ambaye anahusika na maswala ya umoja wa mataifa na mambo ya amani