Shirika
la Afya Dunia (WHO) limetengua uteuzi wa Rais wa Zimbabwe, Robert
Mugabe kuwa Balozi Mwema wa Magonjwa Yasiyoambukiza (NCDs) barani Afrika
kutokana na malalamiko ya watu mbalimbali wakielezea kutoridhishwa na
uteuzi huo.
Katika
taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya shirika hilo, Mkurugenzi Mkuu
wa WHO, Tedros Adhano amesema kuwa, kwa siku chache zilizopita,
nimefiriki kuhusu uteuzi wangu wa Mhe. Mugabe kama balozi mwema, na
baada ya kutafakari kwa kina, nimeamua kutengua uteuzi huo.
"Nimesikiliza
kwa kina mawazo ya wote walioeleza kuhusu kutoridhishwa kwao na uteuzi
huo, na nimesikiliza madai mbalimbali yaliyoibuliwa. Pia nimewasiliana
na serikali ya Zimbabwe, na tukafikia kwenye hitimisho kuwa uamuzi huu
ni bora kwa manufaa ya shirika letu, "aliandika Tedros Adhano.
Baadhi
ya watu waliokosoa uteuzi huo wa Rais Mugabe walisema kuwa, katika
kipindi cha miaka 30 cha uongozi wa Rais Mugabe, mfumo wa afya wa taifa
hilo umeporomoka pakubwa.
Wakosoaji
walisema kuwa hospitali hazina dawa, watumishi wa afya wakati mwingine
hawalipwi stahiki zao, na kiongozi huyo aliyekaa madarakani tangu uhuru,
husafiri nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
Licha
ya kutengua uteuzi huo, Tedros amesema kuwa, bado yupo kwenye nafasi ya
kufanya kazi na nchi yeyote na kwamba wapo tayari kushirikiana na mtu
yeyote katika kujenga mfumo wa afya ulio imara.
Aidha,
amewashukuru wote waliotoa mawazo yao kuhusu uteuzi huo na kusema kuwa,
anategemea ana mijadala ya kujenga ili kuweza kutekeleza majukumu
aliyochaguliwa kuyafanya.
0 comments:
Post a Comment