Thursday, August 20, 2015

JAMES MBATIA ANENA KUHUSU SWALA LA DR. SLAA NA KUZINDUA KAMPENZI ZA UKAWA KATIKA UWANJA WA TAIFA

James Mbatia ni mmoja wa Viongozi wa Umoja wa UKAWA, ambaye  jana   alikutana na Waandishi wa Habari kwenye Ofisi za Makao Makuu ya NCCR- Mageuzi, Ilala Dar

Miongoni  mwa  mambo  aliyoyazungumzia  ni UKAWA kuzuiwa kutumia Uwanja wa Taifa kwenye uzinduzi wa Kampeni zao,  na kutoonekana kwa Dk. Slaa .

“Kampeni zinaanza nawasihi Wanasiasa wote wachunge ndimi zao sana, tujadili hoja kwa hoja kwenye majukwaa ya kisiasa sio kujadili watu, matusi, wala kupigana ngumi au kumwaga damu… 
 
"Tume ya Uchaguzi ambayo ndio refa itende haki pamoja na vyombo vya dola… Wakitenda haki hakuna mgogoro wa aina yoyote, Kamati za Ulinzi na Usalama Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya hatutaki waingilie mchakato huu.“ alisema  Mbatia

Kuhusu kuzuiwa Uwanja wa Taifa Dar, Mbatia  alisema; “Uwanja wa Taifa ni mali ya Watanzania, tutakutana tutatafakari alafu tukishakubaliana kwa pamoja tutatoa taarifa wapi tutakutana na tutazungumza nini, kwa kweli hatuna majibu mpaka sasa hivi,"

Kuhusu swala la Dk. Slaa kutoonekana kwenye Vikao vya UKAWA, Mbatia  alisema;
 “UKAWA sio Mbatia, sio Slaa sio Lipumba sio Mbowe… tusijadili watu tujadili hoja za msingi za taifa, watu wanapita, tuzungumzie Watanzania zaidi“
 
SHUDATE BLOG

0 comments:

Post a Comment