Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ameapishwa kuanza muhula mpya. Katika
hotuba yake, Bw Nkurunziza ameahidi kumaliza ghasia nchini mwake katika
kipindi cha miezi miwili. Maafisa wawili wa ngazi ya juu, akiwemo mkuu
wa zamani wa ujasusi wameuawa katika mashambulio tofauti mwezi uliopita,
baada ya uchaguzi uliokuwa na utata. Mwanaharakati mmoja wa haki za
binaadam pia alipigwa risasi na kujeruhiwa. Kulikuwa na jaribio la
kumpindua Rais Nkurunziza mwezi Mei.
Thursday, August 20, 2015
Home »
» Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ameapishwa
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ameapishwa
5:42 AM
No comments
0 comments:
Post a Comment