Thursday, August 20, 2015

TANGAZO KWA WANA CUF

The Civic United Front (CUF-Chama Cha Wananchi) kinawatangazia na kuwaalika Wazanzibari wote kushiriki katika Mkutano wa hadhara siku ya Jumapili, tarehe 23.08.2015.
Mkutano huo wa aina yake utafanyika katika viwanja vya Kibanda maiti, Unguja kuanzia saa nane kamili mchana hadi saa kumi na mbili jioni (08:00-12:00) na kuhutubiwa na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.
Tukumbuke kwamba Jumapili, ya tarehe 23.08.2015 ni siku maalum, katika eneo màalum kwa ajili ya shughuli maalum.
Shime wazanzibari wote tujitokeze kwa wingi na tuungane kwa pamoja katika siku hii ya kihistoria kwa lengo la kuudhihirishia ulimwengu kuwa hakuna wa kumshinda simba wa nyika, Maalim Seif Sharif Hamad, katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2015.
Atakaesoma tangazo hili asambaze kwa mwengine. Hakuna Kulala..!

0 comments:

Post a Comment