Masaa machache yaliyopita Korea Kaskazini imerusha makombora aina ya rocket na kuipiga Korea kusini na pia wakavipiga vipasa sauti vya Korea Kusini vilivyoko mpakani ambavyo hutumika kusaidia matangazo ya radio, shambulio hilo limejibiwa na Korea Kusini kwa kurusha makombora pia kuelekea Korea Kaskazini, majuzi Korea Kaskazini ilizionya Marekani na Korea Kusini kuacha mara moja mpango wao wa mazoezi ya kijeshi ya pamoja ikisema kama wataendelea na mazoezi hayo itawashambulia wote wawili na tayari imethubutu kuishambulia Korea Kusini ambayo nayo imejibu mapigo kwa kuishambulia pia Korea Kaskazini.
Ngoja tuone na tusubiri mwisho wa hii movie ambayo ikiendelea vita kuu ya tatu ya Dunia itawaka huku nasi tukishuhudia,walio nyuma ya North korea ni China, Russia na Iran.
Source: SHUDATE
0 comments:
Post a Comment