Manchester City wamemsajili beki Nicolas Otamendi kutoka Valencia kwa mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya pauni milioni 32. City watalipa kwanza pauni milioni 28.5 kumpata mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina ambaye alitajwa katika kikosi cha msimu 2014-25 cha La Liga na pia alicheza kwenye fainali ya Copa Amerika.
"Kuwa hapa katika klabu nzuri ni kama ndoto." amesema Otamendi.
Meneja wa Manchester City, Manuel Pellegrini amesema: "Ana nguvu, anaweza kukaba vizuri sana, na ni mzuri kiufundi."
0 comments:
Post a Comment