Lori lenye usajili wa serikali ya Kenya,
GK lilokuwa likisafirisha raia wa Ethiopia karibu 100 liliposhikwa na
polisi katika eneo la Kangeta, Kaunti ya Meru Agosti 18, 2015.
Picha/DAVID MUCHUI
Kamishna wa polisi Kaunti ya Marsabit Bw Peter Thuku alielezea Taifa Leo kuwa lori hilo lilikuwa la kundi la kukabiliana na wizi wa mifugo na halikupewa idhini la kutoka kambini.
Kamishna wa polisi Kaunti ya Marsabit Bw Peter Thuku alielezea Taifa Leo kuwa lori hilo lilikuwa la kundi la kukabiliana na wizi wa mifugo na halikupewa idhini la kutoka kambini.
Bw Thuku alikanusha madai kuwa dereva wa lori hilo aliyetoroka alikuwa polisi.
Aliongeza kuwa afisa wa polisi William Kipchirchir aliyenaswa na
kupelekwa Kortini eneo la Maua kaunti ya Meru alitumia raia kuendesha
lori hilo.
Bw Thuku alitibitisha kuwa dereva wa lori hilo alikuwa likizo.
Alisema kuwa lori hilo lilitumia barabara la kutoka Kaunti ya Wajir
likapitia vichakani kabla ya kuingia Kaunti ya Isiolo na Meru.
“Afisa huyo amekiuka sheria. Tunashangaa kuwa afisa wa polisi anaeza
toroka na gari la kituo cha polisi. Alitumia njia ambalo halikuwa na
maafisa wa polisi. Hii ni uhalifu na sheria lazima ichukue mkondo wake,”
alisema.
Alikashifu kisa hicho akidai kuwa ni utumiaji mbaya wa gari la serikali.
Aliongeza kuwa kushikwa kwa askari wa polisi huyo inafaa iwe funzo kwa
wengine wote.
Kamishana huyo alidai kuwa wakimbizi wamekwepa kutumia barabara ya
Marsabit kwa maana kuna maafisa wa polisi wengi anbao wameshika doria.
Kukwepa maafisa wa trafiki
Gari la polisi lilinaswa Kangeta katika Kaunti ya Meru Jumanne
lilipojaribu kukwepa maafisa wa trafiki huku likiwa limebeba raia wa
Ethiopia.
Mkazi mmoja aliwajulisha maafisa wa polisi kabla ya gari hilo kuzuiliwa.
Raia hao waliojificha ndani ya hema iliyotumiwa kufunika lori hilo, walisema walikuwa wanaelekea Afrika Kusini kutafuka kazi.
Raia hao wa Ethiopia 78 walifikishwa Kortini na kufungwa kwa miezi
mitatu and kuachiliwa kwa dhamana ya Sh50,000 kila mmoja kabla ya
kurudishwa nchini kwao. Wawili wao hawakuweza kufika mahakamani kwa kuwa
walikuwa wagonjwa.
0 comments:
Post a Comment