Friday, September 4, 2015

BONDIA JACOB MAGANGA NDANI YA ULINGO NCHINI HUNGARY SIKU YA KESHO



BONDIA Jacob Maganga anatarajiwa kupanda ulingoni kesho dhidi ya bondia wa Hungary, Nobert Nemesapati kuwania mkanda wa dunia katika pambano la Light heavy weight litakalopigwa kwenye mji wa Sportcsamok nchini humo.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Chama cha Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST) Antony Rutta, Maganga akiongozana na kiongozi wa msafara Emmanuel Mlundwa walitarajiwa kuondoka jana jioni kuelekea Hungary kwa ajili ya pambano hilo la kimataifa.
“Maganga na Mlundwa wataondoka leo (jana) kwenda Hungary, amejiandaa vizuri na tuna imani kubwa hatatuangusha kwani amefanya maandalizi mazuri kuhakikisha anapeperusha vyema bendera ya Tanzania,” alisema.
Maganga atapigana raundi 12 katika uzito wa light heavy unaotambuliwa na Global Boxing Union. Bondia huyo anayetokea Tanga amecheza mapambano 11 na kati ya hayo ameshinda sita kwa ‘Knockout’, amepoteza mawili na kupata sare tatu.
Pia, kutoka kwenye tovuti ya Box Rec, Maganga mwenye umri wa miaka 24 anashika nafasi ya 87 kati ya mabondia 1,022 kwa viwango vya dunia huku kwa upande wa Tanzania akishika nafasi ya pili kati ya 27. Aliwahi kumshinda Mada Maugo, Alibaba Ramadhani, Obeid Buta, Zumba Kukwe, Ally Boznia na Kibonge Issa.

SHUDATE BLOG

0 comments:

Post a Comment