Timu za Uingereza za Man United na Man City zimeanza vibaya michuano ya kombe la klabu bigwa barani Ulaya baada ya kuchapwa. Man United wakiwa ugenini nchini Uholanzi wamelala kwa kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Psv.Memphis Depay alianza kuifungia timu yake bao la kwanza kabla ya Héctor Moreno wa PSV kusawazisha kisha Luciano Narsingh akifunga bao la ushindi.Man City nao wakiwa katika Dimba lao la Etihad walikubali kipigo cha mabao 2-1 toka kwa vibibi vizee ya Turin Juventus mabao ya Juve yakifungwa na Álvaro Morata na Mario Mandzukic huku bao la kujifunga la beki Giorgio Chiellini,likiwapa Man City bao moja.Real Madrid wakiwa nyumbani Santiago Bernabeu wameshinda kwa kishindo kwa ushindi wamabao 4-0 dhidi ya Shakt Donetsk, Cristiano Ronaldo akifunga hattrick na Karim Benzema akifunga bao moja.
Matokeo mengine ya michuano hii ni:
Psg 2 – 0 Malmö FF
VfL Wolfsburg 1 – 0 CSKA
Benfica 2 – 0 FC Astana
Galatasaray 0 – 2 Atletico Madrid
Sevilla 3 – 0 Borussia Mönchengladb
SHUDATE BLOG
0 comments:
Post a Comment