Sunday, September 20, 2015

MABASI 138 YA MRADI WA BRT YAWASILI DAR


TATIZO la usafiri katika Jiji la Dar es Salaam linatarajia kupungua baada ya mabasi 138 ya Mradi wa mabasi Yaendayo Haraka (BRT) unaotarajiwa kuanza kazi Oktoba 2 mwaka huu kuwasili katika Bandari ya Dar es Salaam yakitokea China.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki amekuwa mmoja wa mashuhuda, baada ya kujionea mabasi hayo alipotembelea Bandari ya Dar es Salaam jana. Akizungumza baada ya kuyaona bandarini Dar es Salaam, alisema: “Tumefikia hatua nzuri na naipongeza Kampuni ya UDA Rapid Transit (UDART) kwa kuleta mabasi hayo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma hii ya usafiri katika kipindi cha mpito.
Hii itasaidia kuondoa adha ya usafiri kwa wakazi wa jiji hili.” Alisema kampuni hiyo imepewa jukumu la kuendesha kipindi cha mpito ili waweze kupata uzoefu na zabuni ya mwendesha mradi kipindi cha kudumu itakapo tangazwa itasaidia wao kushindana.
Aliongeza kuwa, Serikali ilifanya kazi kubwa kuunganisha Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam na wamiliki wa daladala na baadaye kuanzisha kampuni ya UDART. Aidha alikanusha kuwa nauli za mabasi hayo imepangwa kuwa Sh 900 zilizotolewa katika mtandao, na kusema huo ni uzushi na upotoshaji na aliyefanya hivyo anatafutwa ili sheria ichukue mkondo.
Alisema suala la nauli linahusisha ushiriki wa taasisi mbalimbali chini ya Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) hivyo uzushi huo umewaletea usumbufu mkubwa wakazi wa Dar es Salaam hivyo wanatakiwa kuwapuuzia.
Msemaji wa Kampuni ya UDA Rapid Transit (UDA-RT), Sabri Mabrouk alisema mabasi yote yameingia yakiwemo ya meta 12 yapo 101 na meta 18 yapo 39 na huduma ya usafiri kipindi cha mipito itanza baada ya kukamilisha taratibu za bandari.
“Tuliahidi kuwa mwezi huu wa tisa mabasi yatakuwa yamewasili na ni kweli yamekuja,” na kwa pamoja na yale ya kufundishia yatakuwa mabasi 140,” alisema Mabrouk. Alifafanua kwamba mabasi hayo yametokea kiwandani China na yanakidhi miundombinu ya barabara ya mradi wa BRT kama walivyokubaliana.

SHUDATE BLOG

Related Posts:

  • WATU WAWILI WAFARIKI KWA AJALI YA GARI MKOANI IRINGA Gari aina ya Toyota Harrier likitolewa eneo la ajali. Wananchi wakishuhudia gari hilo wakati likiondolewa eneo la ajali. Wanausalama wakiwa eneo la ajali. Toyota Harrier likiwa limeharibika vibaya baada ya ajali hiy… Read More
  • KESI YA KUPINGA SHERIA YA MTANDAO YAANZA RASMI Mchakato wa usikilizwaji wa kesi ya Sheria ya Makosa ya Uhalifu wa Kimtandao umeanza, huku Mahakama Kuu nchini ikiipa Serikali siku 14 kuwasilisha mahakamani hapo majibu yake ya utetezi kuhusiana na kesi hiyo. Kesi hiyo… Read More
  • AJALI YA BASI LA METRO WATU watano wamekufa papo hapo na wengine 39 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la Kampuni ya Metro, kuacha njia, kutumbukia bondeni na kupinduka. Basi hilo lilikuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Rombo mkoani Kilimanjaro. Mi… Read More
  • KAZI INAENDELEA VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mabingwa watetezi, Yanga, leo watakuwa tena kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania pointi tatu dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya katika mechi ya raundi ya pili ya ligi hiyo. Yang… Read More
  • UDOM--TARATIBU ZA UJAZAJI WA FOMU YA BIMA YA AFYA Wanafunziwa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) mna taarifiwa kwamba kuanzia mwaka huu wamasomo (2015/2016), mtawajibika kuchangia katika Mfuko wa bima ya afya ya taifa(NHIF). Wanao paswa kulipia ni wale wote wasio kuwa na kadi … Read More

0 comments:

Post a Comment