Tuesday, September 1, 2015

WALICHOKIFANYA CHELSEA KWA PEDRO NA MANCHESTER WAMEFANYA TENA KWA CRYSTAL PALACE

COVER

John Stones alikua changuo la kwanza kwa Chelsea ili kuimarisha sehemu ya ulinzi wa goli lao, lakini jaribio hilo limeshindikana baada ya Everton kukataa pesa zao nyingi.
Sasa ukikosa A unaenda kwa B, John Stones imeshindikana na Chelsea wamemsaini beki mwenye miaka 23 Michael Hector kutoka Reading kwa gharama ya £4.5m. Crystal Palace walionyesha kutaka kumsajili beki huyo raia wa Jamaica leo asubui lakini kama walivyofanyiwa Manchester kwa Pedro, imefanyika tena kwa Crystal Palace. Chelsea walifika mbele ya Crystal na kumsajili mchezaji huyo na kuwaacha Palace.
Michael Hector ni shabiki wa Chelsea kwasababu alikua ana post picha zake akiwa amevaa jezi ya Chelsea kwa muda mrefu. Kwake yeye kujiunga na Chelsea ni dream come true.
Hector alikua kwenye mkopo ndani ya timu 11 kabla ya kujiunga na Chelsea. The Blues wameruhusu magoli 9 kwenye mechi nne ambazo pia wameambulia point 4. Wanahitaji sana kuimarisha sehemu yao ya ulinzi wa goli.
SHUDATE BLOG

1 comment: