Friday, September 4, 2015

MH. MIZENGO PINDA ATOA USHAURI KWENYYE SEKTA YA UWEKEZAJI NCHINI

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema wakati Tanzania inajiandaa kutekeleza awamu ya pili ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016 -2020) ambao unalenga kukuza viwanda nchini, haina budi kuangalia ni aina gani ya uwekezaji unafaa kuchukuliwa kwa manufaa ya nchi.
Alitoa kauli hiyo juzi usiku wakati akizungumza na mabalozi na wageni mbalimbali waliohudhuria maadhimisho ya miaka 70 ya Uhuru wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam na miaka 50 ya kuanzishwa kwa mahusiano ya kidiplomasia baina ya Tanzania na Vietnam, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
“Huu ni wakati muafaka kwa nchi zetu kuangalia ni aina zipi za uwekezaji zinafaa kuchukuliwa kwa manufaa ya nchi zetu na wananchi wake. Nitumie fursa hii kuwakaribisha wawekezaji kutoka makampuni ya Ki-Vietnam waje kuwekeza kwenye usindikaji wa korosho, utengenezaji wa saruji na viwanda vya nguo,” alisema Waziri Pinda.
Aliyataja maeneo mengine ambayo wenye kampuni wanaweza kuwekeza kuwa ni nyanja ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) pamoja na ujenzi wa nyumba za kuishi.
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuipongeza kampuni ya mawasiliano ya simu ya Vietnam (VIETTEL) kwa uamuzi wake wa kutenga Dola za Marekani bilioni moja ambazo zitatumika kuendesha shughuli zake nchini.
“Huu ni mtaji mkubwa sana, siyo tu hapa Afrika Mashariki na Kati bali hata barani Asia. Uwekezaji huu utazalisha ajira za moja kwa moja 1,700 na ajira nyingine 20,000 ambazo si za moja kwa moja,” aliongeza.
Kwa upande wake, Balozi wa Vietnam nchini Tanzania, Vo Thanh Nam alisema tangu ipate uhuru wake hadi, nchi hiyo imekwishaanzisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi 185 na wakati huo huo imekwishaweka uhusiano wa kibiashara na uwekezaji na nchi 220.
SHUDATE BLOG

Related Posts:

  • 20 MOST UNIQUE BUILDING IN ASIA Largest and most populous continent Asia is notable for its unusually dense and large settlements. Some of the buildings in Asia are innovative, experimental and unique. Many of these strange buildings are in China. Her… Read More
  • HALI SIO NZURI BUKINA FASO Rais wa mpito wa Burkina Faso Michel Kafando amepokonywa wadhifa wake na serikali yake kuvunjwa. Jumuia ya kimataifa imelaani mapinduzi hayo yaliyotokea chini ya mwezi mmoja kabla ya uchaguzi mkuu. Kasri la rais mjini Oua… Read More
  • THE MOST TALLEST BUILDING IN THE WORLD RankBuilding[A][9]CityCountryHeight (m)[3]Height (ft)FloorsBuilt 1Burj Khalifa†Dubai UAE828 m2,717 ft1632010 2Shanghai TowerShanghai China632 m[10]2,073 ft1232015 3Abraj Al-Bait Clock TowerMe… Read More
  • MOST TALLEST BUILDING IN AFRICA BuildingPinnacle HeightFloorsYearCountryCity Carlton Centre223 m (732 ft)501973 South AfricaJohannesburg Ponte City Apartments173 m (568 ft)541975 South AfricaJohannesburg UAP Tower[3][4]163&n… Read More
  • MOST TALLEST BUILDING IN TANZANIA #NameImageCityHeight (≈ m)FloorsYear 1PSPF Commercial Twin TowersDar es Salaam152.80352014 2Rita TowerDar es Salaam123302014 3Uhuru HeightsDar es Salaam102.6272012 3Millennium TowerDar es Salaam-302014 4Umoja wa Vijana Co… Read More

0 comments:

Post a Comment