Mlipuko mkubwa umetokea katika kambi moja ya wakimbizi wa ndani, mjini Yola, mji mkuu wa Jimbo la Kaskazini Mashariki la Adamawa.
Mashirika ya kutoa misaada ya dharura yamethibitisha mlipuko huo na kusema kuwa maafisa wa polisi wameuzingira eneo hilo kwa sasa.
Mlipuko huo ulitokea katika chumba kimoja cha kuhifadhi vyakula katika kambi ya Malkohi.
Haijabainika nini kilisababisha mlipuko huo na ni wakimbizi wangapi wameathirika.
Ripoti zinasema kuwa zaidi ya watoto 1000 walikuwa katika kambi hiyo, iliyojengwa kuwahifadhi watu waliokimbia makwao kutokana na uasi unaoendelea Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Maafisa wa shughuli za uokozi wametumwa katika eneo hilo huku uchunguzi ukiendelea.
0 comments:
Post a Comment