Friday, September 11, 2015

WANAJESHI WA CAMEROON WASITISHA MGOMO

Wanajeshi wa Cameroon, ambao wamekuwa kwenye mgomo baridi, kulalamikia kutolipwa mishahara yao, baada ya kuhudumu katika kikosi cha Umoja wa Mataifa, katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, wamesitisha mgomo.
Image copyrightAFP
Image captionJeshi la Cameroon
Ripoti zinasema kuwa mgomo huo ulisitishwa baada ya serikali kuwalipa wanajeshi hao mishahara yao.
Wanajeshi hao walipiga kambi katika makao makuu ya jeshi mjini Yaunde hiyo jana wakitaka kulipwa mishahara yao.
Raia walizuia kutumia njia inayopita karibu na kambi hiyo ya jeshi wakati wa mgomo huo.
Image copyrightAFP
Image captionJeshi la Cameroon nchini CAR
Kulikuwa na msongamano mkubwa wa magari mjini humo baada ya barabara nyingi zinazoelekea katika shule kadhaa zilizokaribu na kambi hiyo kufungwa.
Wanajeshi hao walianza maandamano hayo kutoka chuo cha mafunzo ya kijeshi kisha wakatembea hadi kati kati mwa mji mkuu na hatimaye kuelekea ofisi ya waziri mkuu, ambayo pia ni makao makuu ya wizaya ya ulinzi.
Kisha wanajeshi hao walielekea moja kwa moja hadi majengo ya bunge ambako walielezea kutoridhishwa kwao na wakuu wao.
Image copyrightAFP
Image captionWanajeshi wa MINUSCA
Jeshi hilo limekuwa likihudumu nchini CAR chini ya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini humo maarufu kama MINUSCA, tangu kwa wa 2014.
Cameroonm ilituma wanajeshi 850 nchini humo na kila mmoja wao alikuwa akipokea mshahara ya dola elfu moja kila mwezi, lakini wengi wanadai kuwa walipokea nusu ya mshahara huo wakati huo wote.
SHUDATE BLOG

0 comments:

Post a Comment