Watoto wawili wa familia moja wamekufa maji baada ya mtumbwi waliokuwa wakitumia kuvulia samaki, kugonga mwamba na kuzama katika Ziwa Victoria.
Akithibitisha tukio hilo la juzi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi alisema siku ya tukio, majira ya saa moja jioni watoto hao waliiba mtumbwi na kuingia nao Ziwa Victoria eneo la kisiwa cha Bumbile kwa lengo la kuvua samaki.
Alifafanua kwamba wakati wakiendelea na uvuvi, ghafla mtumbwi wao uligonga mwamba na kusababisha watoto hao kuzama na kufa maji.
Aliwataja watoto hao kuwa ni Andisius Masenene aliyekuwa anasoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Bumbile na mdogo wake, Rugumisa Masenene aliyekuwa anasoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi ya Bumbile. Kamanda alisema umri wao haujafahamika.
Kwa mujibu wa Mtendaji wa Kata ya Bumbile, Herman Mgango, mwili wa Andisius ulipatikana na kwamba mwili mwingine unaendelea kutafutwa.
SHUDATE BLOG
0 comments:
Post a Comment