Thursday, September 3, 2015

Rais Omar al-Bashir ziarani China

Rais wa Sudan Omar al-Bashir na mwenzake wa China, Xi Jinping

Wizara ya mambo ya kigeni ya China imesema imetoa mualiko kwa Bashiri ili ahudhurie sherehe za kuadhimisha miaka miwili ya kumalizika vita vya pili vya dunia. Bashir ni mmoja wa viongozi wa kigeni watakaohudhuria gwaride kubwa la kijeshi siku ya Alhamisi kuadhimisha miaka 70 ya Japani kusalimu amri katika vita vikuu vya pili vya dunia. Hata hivyo viongozi wakuu wa Mataifa ya Magharibi wamejitenga na sherehe hizo.
"Wewe ni rafiki wa zamani wa watu wa China, China na Sudan ni kama kaka wawili, ambao ni marafiki na washirika wa kweli. Bwana Bashiri kuja China inaonesha ushirikiano wetu ni wa nguvu," alisema rais Xi aliposalimiana na mwenzake wa Sudan aliyekuwa ameandamana na ujumbe wake. Bashir alisema amefurahi kupata mualiko wa kuhudhuria gwaride hilo la kijeshi ambapo vikosi 12,000 vitapita kati kati ya mji wa Beijing.
Aidha, wizara ya mambo ya kigeni ya China imejitetea baada ya baadhi ya ripoti kusema kumualika mtu anayekabiliwa na uhalifu wa kivita katika sherehe hizo zinazotajwa kuwa za amani ni kupingana na kile kinachosherehekewa.
Wizara hiyo imesema watu wa Afrika wakiwemo watu wa Sudan wana mchango mkubwa katika vita hivyo vya kupinga mafashisti wakitumia jina la serikali ya China katika vita vya pili vya dunia. Msemaji wa wizara hiyo Hua Chunying ameeleza nchi yake haikutia saini mkataba w aroma unaounda mahakama hiyo kwahiyo hawalazimiki kumkamata.
Mahakama hiyo ya Kimataifa ICC ilioko mjini The Hague Uholanzi, ilitoa waranti wa kukamatwa kwa Bashir mwaka wa 2009 na 2010, ikimshutumu kupanga mauaji ya kimbari na visa vengine vya kikatili Magharibi mwa Darfur. Bashir amekuwa akisafiri mara kwa mara kwa nchi jirani na Sudan lakini amejiepusha na ziara za mbali zitakazomuweka katika hatari ya kukamatwa.
Hapo Jumatatu Marekani ilielezea wasiwasi wake juu ya ziara ya Bashiri nchini China huku msemaji wa wizara ya mambo ya nje Mark Toner akisema nchi hiyo inapinga mualiko, ufadhili au usaidizi wa aina yoyote kwa mtu ambaye waranti wa kukamatwa kwawe imetolewa na mahakama ya ICC.

SHUDATE BLOG

Related Posts:

  • Ghasia zaendelea kwenye eneo la Msikiti wa Al-Aqsa Leo ni siku ya tatu tangu mapambano yaanze baina ya polisi na Waislamu kwenye eneo la msikiti wa Al-Aqsa Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Rais, Bwana Erdogan amemwambia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki-moon kwa … Read More
  • HALI BADO NI NGUMU KWA WAKIMBIZI ULAYA Mamia ya wahamiaji wako katika hali ya sintofahamu katika eneo la mpaka wa Serbia na Hungary baada ya Serikali ya Hungary kufunga mpaka wake kwa uzio. Hatua hiyo inadhumuni la kuwazuia wahamiaji wanaojaribu kuingia katika… Read More
  • VPL LEO INAENDELEA Ligi Kuu Tanzania bara Itaendelea tena leo katika viwanja saba ikiwa ni michezo ya mzunguko wa pili. Mabingwa watetezi wa kombe hilo klabu ya Young Africans watakuwa wenyeji wa Tanzania Prisons katika uwanja wa Taifa jijin… Read More
  • Merkel aitisha mkutano kujadili mgogoro wa wakimbizi Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameitisha mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya wiki ijayo kuhusu mgogoro wa wakimbizi, akisema suluhu ya pamoja inahitajika ili kukabiliana na mgogoro huo uliyougawa Umoja wa Ulaya. Kansel… Read More
  • UEFA : MAN UNITED NA MAN CITY ZAANZA VIBAYA Timu za Uingereza za Man United na Man City zimeanza vibaya michuano ya kombe la klabu bigwa barani Ulaya baada ya kuchapwa. Man United wakiwa ugenini nchini Uholanzi wamelala kwa kichapo cha mabao 2-1 dhidi… Read More

0 comments:

Post a Comment