KOCHA wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ametamba washambuliaji wake wakiongozwa na Jeryson Tegete watatisha hivyo kila timu ijiandae kupata kipigo.
Mshambuliaji huyo zamani wa Yanga ametua katika timu hiyo inayotarajia kucheza kwa mara ya kwanza ligi kuu Bara msimu huu.
“Tofauti na watu wengi wanavyoamini kuhusu uwezo wa Tegete ambaye katika misimu yake minne ya mwisho katika timu ya Yanga alikuwa ‘mkosa magoli aliyezoeleka lakini klabu zetu kubwa zimejaa majungu, Tegete ana kiwango kikubwa na nitamsaidia kumrejesha katika makali yake ya ufungaji,” alisema Julio.
shudate blog
0 comments:
Post a Comment