Wednesday, September 2, 2015

Bunge la Guatemala limepiga kura jana kumuondolea kinga ya kutoshtakiwa rais Otto Perez Molina

Image result for otto perez molina

Bunge la Guatemala limepiga kura jana kumuondolea kinga ya kutoshtakiwa rais Otto Perez 
Molina, na hivyo kumuweka katika uwezekano wa kushtakiwa kuhusiana na kashfa ya rushwa 
iliyoutikisa utawala wake na mfumo wa kisiasa wa nchi hiyo.Wabunge wote 132 waliokuwepo bungeni kati ya 158 waliunga mkono hatua hiyo ya kihistoria, 
na hivyo kuwafungulia njia waendesha mashtaka kumshtaki rais Perez Molina kama raia 
yeyote wa kawaida, na jaji anaweza kuamuru awekwe kizuwizini.
Serikali ya Perez inatuhumiwa kwa kuhusika na matukio kadhaa ya rushwa, lakini mpaka 
wakati huu imekuwa ina kinga ya kutoshtakiwa. Maafisa nchini Guatemala wamesema rais 
huyo amezuwiwa kuondoka nchini humo.Perez Molino mwenye umri wa miaka 64 anasisitiza kutohusika na vitendo vyovyote vya rushwa, na ameapa kupambana mahakani kujisafisha.

SHUDATE BLOG


0 comments:

Post a Comment