Kuelekea kwenye mechi muhimu ambayo Liverpool wanayo dhidi ya Manchester united Jumamosi hii, lazima watamkumbuka captain wao Steven Gerrard. Captain wao alikua na uzoefu uwanjani, anaongoza kwa mfano akicheza kwa nguvu zote ili timu ishinde. Lakini kwa sasa hayupo tena na mechi itachezwa kama kawaida na wanaitaji ushindi bila ya yeye kuwepo.
Steven Gerrard amesema kwamba angeweza kubaki Liverpool kama angepata ofa ya tofauti kidogo. Kuna wakati mchezaji kama yeye anahitaji zaidi ya mkataba mpya wa pesa. Gerrard anasema “Nilishangazwa kwanini wakati wa mazungumzo na agent wangu, cheif executive wa club hakutaja majukumu ya kumsaidia kocha lakini labda itatokea siku moja. Nimekaa kama mchezaji kwenye timu kwa muda nikiongoza wenzangu, labda ningepata nafasi ya kujifunza zaidi kuhusu ukocha na management ingekua kitu cha ziada kwangu. Niliondoka wakati milango ipo wazi lakini bado ingewezekana kuwa Liverpool sasa hivi. Lakini kwanini Liverpool isingenifanyia mimi kama Manchester ilivyomfanyia Ryan Giggs”
Pia Gerrard anakubali kwamba amei-miss ligi ya kwao England,“Ndio nai-misss sana, na miss kila kitu kuhusu EPL. Naangalia TV kuona mechi zikiwa na mashabiki elfu 50, 60 hadi 70. Hali na ushindani kuhusu hilo nakubali kuwa namiss sana EPL”.Steven Gerrard anajiandaa kutoa kitabu chake ambacho amezungumza mambo mengi kuhusu maisha yake ya soka hadi anahamia ligi ya Marekani.
0 comments:
Post a Comment