Tuesday, September 8, 2015

TIKETI ZA VISHINA KUENDELEA KUTUMIKA VPL 2015/16

tff_LOGO1

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeendelea kujiaibisha baada ya jana kueleza kuwa litatumia tiketi za mfumo wa kizamani za vishina kwenye mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu.

Msimu huu wa ligi hiyo utaanza rasmi Septemba 12 ukishirikisha timu 16 kutoka mikoa tisa ya Tanzania Bara.

Baraka Kizuguto, Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwa wataendelea kutumia tiketi za vishina hadi pale kasoro zilizojitokeza katika mfumo wa kisasa wa tiketi za elektroniki zitakaporekebishwa.

“Tiketi za elektroniki hazikusitishwa na TFF, zilisitishwa na serikali. Tutaendelea kutumia tiketi za kawaida msimu huu hadi pale wahusika watakapokubaliana kurejea kwenye mfumo wa tiketi za kielektroniki baada ya kurekebisha kasoro zilizojitokeza msimu uliopita,” alisema Kizuguto.

SHUDATE BLOG

0 comments:

Post a Comment