Tuesday, September 15, 2015

Mafuriko Nyumba ya Mungu yasomba ekari 20



ZAIDI ya ekari 20 za mazao ya aina mbalimbali, ikiwamo vitunguu na mahindi pamoja na nyumba ambazo idadi yake haijulikani katika vijiji vya Jitengeni na Mvungwe wilayani Same, zimeharibiwa na mafuriko kutoka bwawa la Nyumba ya Mungu.
Wakizungumza na waandishi wa habari, baadhi ya wakazi wa vijiji hivyo, Zuhura Mushi na Joseph Makongoro walisema maji hayo yaliingia katika makazi na mashamba yao tangu Septemba 8 mwaka huu majira ya saa 2.00 usiku.
“Haya maji yamesababisha hasara ya mamilioni ya fedha kwani mashamba ya vitunguu, maharage na mahindi yalifikia hatua ya kuvunwa lakini sasa yanaonekana kutaka kuoza,” alisema Makongoro.
Mkuu wa Wilaya ya Same, Herman Kapufi pamoja na kukiri kuwapo kwa mafuriko hayo, lakini alifafanua hayakusababishwa na mvua, bali maji kutoka bwawa la Nyumba ya Mungu.
Kaimu Ofisa wa Maji wa Bonde la Pangani (PBWO), Jereboam Riwa alisema mafuriko hayo yalisababishwa na Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kufungua maji katika bwawa hilo bila kufuata utaratibu.
SHUDATE BLOG

0 comments:

Post a Comment