Wednesday, September 2, 2015

Mwalimu Mkuu shule ya Msingi Mtunguja afariki dunia


 Image result for sad news

Niko hapa Hospitali ya Wilaya ya Same, naona watu wanamiminika kwa wingi baada ya Mwalimu,Ntarishwa Samweli Vianga (63), kufariki dunia jana kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kupigwa na watoto wake wawili waliotajwa kwa majina ya Kachuchu (27) na Kitoi (22).
Huyu ni Mwalimu mwenzetu alikuwa ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Mtunguja iliyopo Kata ya Vudee - Same mkoani Kilimanjaro lakini leo nimefika hapa mjini kuchukua mshahara ndio nakakutana na hizi habari ikabidi nije nithithibishe taarifa hizi nikakuta huyu ndugu yetu hatunaye tena.
Majirani zake hapa hospitalini wanasema chanzo cha tukio kifo cha huyu mwenzetu ni kutofautiana na watoto wake wawili ambao walitaka Baba yao ambaye sasa ni marehemu ampe mmoja wa mtoto aliyetajwa kwa jina la Kachuchu hela kiasi cha shilingi 6,000 kila siku anapokwenda shamba na mwingine aihitaji apewe urithi wa shamba na mali zake ambaye ni mtoto wa mwisho anayeitwa Kitoi.

Lakini pia hao watoto wake wanaelezwa na majirani zake waliopo hapa kuwa wanatumia dawa za kulevya kwa muda mrefu. Jana Septemba mosi, 2015 alipelekwa kutibiwa Hospitali baada ya Mision ya Vudee inayomilikiwa na KKKT Dayosisi ya Pare lakini muda mfupi alipoteza maisha kutokana na kuvuja damu nyingi, pia naambiwa huenda alikuwa na mpresha. 
Juzi ndio marehemu alipigwa na watoto hadi Baba yao kabla hajafa akatoa taarifa kwenye Ofisi ya Kijiji kuwa amewashindwa watoto wake baada ya hapo walikamatwa na Askari na sasa wako hapa Kituoni Same.

SHUDATE BLOG

0 comments:

Post a Comment