Rais Uhuru Kenyatta awapongeza wanariadha wa Kenya walionyakua ubingwa wa dunia katika michezo ya riadha ya dunia huko mjini Bejing kwa kunyakua medali 16 , saba kati ya hizo za dhahabu."Vijana wetu kwa mara nyingine tena wameonesha kwamba wanaweza kufanya vizuri kama wachezaji bora dunia, " amesema Uhuru Kenyatta katika taarifa kwa vyombo vya habari. Amehimiza kuimarishwa kwa mpango wa taifa wa maendeleo ya vijana, kuwapa uwezo vijana wengi wa Kenya ili kuifanya Kenya kuweza kushindana vizuri zaidi katika mashindano ya kimataifa. Kenya ambayo imekuwa ikitamalaki katika mbio za masafa mafupi na marefu, imepata ushindi adimu katika mbio za mita 400 kuruka viunzi na kurusha mkuki mjini Beijing kwa mara ya kwanza.
Asbel Kiprop ameshinda mbio za mita 1,500 kwa mara ya tatu na kunyakua dhahabu na kuihakikishia Kenya kuwa juu ya nchi zilizonyakua dhahabu nyingi katika fainali ya mbio hizo jana Jumapili.Rais wa chama cha riadha nchini Kenya Isaiah Kiplagat , amesema mafanikio hayo yametokana na mipango mizuri katika chama chake.
Kikosi cha wanariadha wanaume wa marekani kimeshinda dhahabu kwa mara ya nne mfululizo katika mbio za mita 400 mara 4 , lakini Mjamaica Novlene Williams-Mills aliweza kukata mbuga na kutokezea wa mwanzo katika mbio kama hizo kwa wanawake akiwashinda wanawake wa Marekani na kujinyakulia medali ya sita ya dhahabu mjini Beijing kwa kikosi cha vigogo hao kutoka katika visiwa vya karibiki.
Vivian Jepkemoi Cheruiyot bingwa wa mita 10,000 duniani
Bingwa wa mita 1,500 mjini Beijing Asbel Kiprop
Vivian Jepkemoi Cheruiyot bingwa wa mita 10,000 duniani
Julius Yegokutoka Kenya bingwa wa kurusha mkuki
SHUDATE BLOG
0 comments:
Post a Comment