Monday, September 7, 2015

Kesi inayomkabili aliyekuwa rais wa Chad, Hissène Habré inaanza kusikilizwa leo

Image result for hissene habre

Siku 45 baadaye mawakili watatu walioteuliwa wamepata muda wa kutosha kuiangalia kesi hiyo lakini mteja wao hawatambui na amekataa kuwasiliana nao.
Jaji wa mahakama ya Burkinabe, Gberdao Gustave Kam ataamua iwapo kesi hiyo itaendelea bila upande wa utetezi wa Hissene Habre.
Tangu mwanzo wa utaratibu wa kesi hiyo, Hissene Habre, mwenye umri wa miaka 72, amekuwa akikataa kutambua uhalali wa mahakama maalum ya Afrika, ambayo iliundwa na Umoja wa Afrika mwaka 2013, ili kushugulikia kesi yake nchini Senegal. Rais huyo wa zamani wa Chad hajawahi kujibu maswali ya jaji.
Afisa wa Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, Reed Brody amesema kwa kukataa kushirikiana na mahakama, Habre anajaribu kuchelewesha utaratibu wa mahakama, ambayo ina bajeti ya Dola milioni 9.5.
Kucheleweshwa kwa kesi hiyo kwa siku 45 kutaongeza bajeti kwa asilimia tisini.
Kesi hiyo ilikadiriwa kuchukua muda wa siku 90 pekee. Waathirika ambao walifanya kampeni ya miaka 25 kuhakikisha ameshtakiwa wanatarajia kuwa mahakama hiyo itatenda haki.
Hii ni mara ya kwanza rais wa nchi kushtakiwa katika nchi nyingine ya Afrika kwa shutma za unyanyasaji, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.
Mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo maalum atajaribu kuwasilisha ushahidi kuonyesha kuwa Habre aliamuru mauaji na unyanyasaji wa maelfu ya watu waliompinga kisiasa.
Tume ya ukweli iliyoundwa kuchunguza madai hayo ilipata ushahidi wa mauaji ya takriban watu 4,000 na ikakadiria kuwa huenda idadi hiyo ikawa mara 10 zaidi.
 shudate blog

Related Posts:

  • Ayew mechazaji bora Uingereza Mshambulizi matata wa klabu ya Swansea City Andre Ayew, ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi uliopita, katika ligi kuu ya Uingereza ya Premier Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ghana mwenye umri wa miaka 25, amefunga mago… Read More
  • WANAJESHI WA CAMEROON WASITISHA MGOMO Wanajeshi wa Cameroon, ambao wamekuwa kwenye mgomo baridi, kulalamikia kutolipwa mishahara yao, baada ya kuhudumu katika kikosi cha Umoja wa Mataifa, katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, wamesitisha mgomo. Image copyrightAFPIm… Read More
  • EMPLOYMENT OPPORTUNITY 1. MEDICAL OFFICER II (5 POSITIONS) Reports to : Head of Firm Duties and Responsibilities • To perform Medical duties in Obstetrics and Gynaecology, Surgery,Anaesthesia Medicine, Paediatrics, Preventive Medicine and … Read More
  • Mataifa ya Ulaya kujadili suala la wakimbizi Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani na Luxembourg wanatarajia kukutana na wenzao wa Jamuhuri ya Czech, Hungary, Poland na Slovakia mjini Prague kwa ajili ya kujadili suala la wakimbizi. Rais wa Halimashauri ya um… Read More
  • Mlipuko mkubwa watokea Yola, AdamawaImage copyrightAPImage captionMaafisa wa shirika la msalaba mwekundu Yola Mlipuko mkubwa umetokea katika kambi moja ya wakimbizi wa ndani, mjini Yola, mji mkuu wa Jimbo la Kaskazini Mashariki la Adamawa. Mashirika ya kutoa m… Read More

0 comments:

Post a Comment