Friday, September 4, 2015

David Cameron kutoa msimamo kuhusu wahamiaji



Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron anatarajiwa kutangaza mipango hapo baadae ya kuongeza idadi ya Wakimbizi kuingia nchini humo.
Hakuna idadi kamili iliyoafikiwa, lakini Cameron alisema Uingereza itaendelea kuwachukua maelfu.
Wakimbizi wengine wanatarajiwa kutoka kwenye Makambi ya Umoja wa Mataifa katika mpaka wa Syria, na si miongoni mwa wale ambao tayari wako Ulaya.
Waziri Mkuu,ambaye amepata shinikizo kuongeza nguvu kushughulikia tatizo la wahamiaji, atatoa kauli yake nchini Uhispania baada ya mazungumzo na Viongozi wenzao.
Cameron anakutana na wenzake wa Portugal na Uhispania kwa ajili ya mazungumzo ambayo yametawaliwa zaidi na maswala ya mzozo wa uhamiaji.
SHUDATE BLOG

0 comments:

Post a Comment