Friday, September 11, 2015

Mataifa ya Ulaya kujadili suala la wakimbizi

Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani na Luxembourg wanatarajia kukutana na wenzao wa Jamuhuri ya Czech, Hungary, Poland na Slovakia mjini Prague kwa ajili ya kujadili suala la wakimbizi.
Rais wa Halimashauri ya umoja wa Ulaya Jean- Claude Junker
Rais wa Halimashauri ya umoja wa Ulaya Jean- Claude Junker
Mataifa ya ukanda huo yalikataa suala hilo la kugawana wakimbizi juma lililopita na kusema kuwa umoja wa ulaya ni lazima utafute chanzo cha mgogoro huoi kwanza ikiwa ni pamoja na kulinda mipaka inayounganisha mataifa hayo kwa kutumia mfumo huru wa hati ya kusafiria ndani ya mataifa yanayounda mkataba wa Shengen na pia kupambana na wafanyabiashara wasafirishaji wa wakikimbizi.
Hata hivyo Ujerumani ambayo iko msitari wa mbele hivi sasa katika kushughulikia suala hilo la wakimbizi imesema kuwa mpango uliowekwa na Rais wa halimashauri kuu ya ulaya Jean- Claude Junker wa kushughulikia suala hilo hautoshi peke yake kwa sasa kutatua tatizo hilo la wakimbizi ambalo ni kubwa zaidi tangu kumalizika kwa vita vikuu vya pili.
Wakimbizi wanaoingia nchini Hungary waongezeka.
Wakimbizi waliowasili nchini Hungary
Wakimbizi waliowasili nchini Hungary
Idadi ya wakimbizi wapatao 3,321 walioingia nchini Hungary hapo jana ni kubwa zaidi kuwahi kutokea ndani ya saa 24, na ilisababisha waratibu wa safari za treni nchini Austria kusimamisha huduma hiyo kwa muda kutokana na msongamano wa abiria katika treni hizo.
Wengi wa wakimbizi wanaharakisha kuvuka mpaka kuingia nchini Hungary kabla ya taifa hilo kuanza utekelezaji wa sheria ngumu dhidi ya wakimbizi ifikapo Septemba 15, hatua ambayo inaonekana kupingwa na shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia wakimbizi.
Inakadiriwa kuwa ifikapo juma lijalo kiasi cha wakimbizi 42,000 watakuwa wameingia nchini Hungary ili kuwahi kabla ya sheria hiyo kuanza kutumika.
Mataifa yanayounda umoja wa ulaya hadi sasa yamegawanyika katika msimamo kuhusiana na jinsi ya kushughulikia na kugawana mzigo huo wa wakimbizi.
Kulingana na utaratibu wa ugawanaji wa idadi ya wakimbizi uliotolewa wiki hii, Ujerumani itapaswa kuchukua zaidi ya wakimbizi 31,000, Ufaransa 24,000 na Uhispania wakimbizi 15,000 wakati Uingereza tayari imeahidi kuchukua wakimbizi 20,000 kutoka nchini Syria walioko katika makambi ya wakimbizi nje ya mataifa yanayounda umoja wa ulaya.
Wakati hayo yakiendelea wabunge wa mataifa ya umoja wa ulaya wamependekeza pia kuwepo kwa kongamano la kimataifa litakalojadili suala la wakimbizi likihusisha mataifa ya Marekani, Umoja wa mataifa na mataifa ya kiarabu.
Akijibu hoja ya kwanini Marekani imekua nyuma katika kusaidia mzigo huo wa wakimbizi, Rais Barack Obama aliahidi kupokea kiasi cha wakimbizi 10,000 wa Syria katika kipindi cha kuanzia Oktoba mosi mwaka huu.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Josh Earnest amesema pia kuwa rais Obama ameagiza kuongeza idadi hiyo ya wakimbizi kutoka nchini Syria kutoka 1,500 baada ya wamarekani 62,000 kusaini waraka wa maombi wa kukubali taifa hilo kupokea wakimbizi zaidi.
shudate blog

Related Posts:

  • SAFARI YA DE GEA MADRID YASHINDIKANA Uhamisho wa Golikipa David De Gea kutoka Manchester United kwenda Real Madrid ya Hispania umekwama dakika za mwisho kwa sababu ya karatasi muhimu za uhamisho kuchelewa . Madrid walikua tayari kutoa dau la pauni milioni 29… Read More
  • DR. SLAA ATAONGEA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI MCHANA HUU Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Dkt. Wilibrod Slaa, leo tarehe 1 Septemba 2015, atavunja ukimya kwa kuongea na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano wake na waandishi wa … Read More
  • KENYA YAONGOZA KWA MEDALI Rais Uhuru Kenyatta awapongeza wanariadha wa Kenya walionyakua ubingwa wa dunia katika michezo ya riadha ya dunia huko mjini Bejing kwa kunyakua medali 16 , saba kati ya hizo za dhahabu."Vijana wetu kwa mara nyingine tena … Read More
  • TAIFA STARS KURUDI NYUMBANI LEO KUTOKA UTURUKI Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajiwa kurejea leo usiku kutoka nchi Uturuki ilikokua imeweka kambi. Taifa Stars iliweka kambi ya wiki moja kujifua na mchezo wake dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria hapo Se… Read More
  • Watson, Ivanovic wachapwa US Open 2015 Muingereza Heather Watson amepoteza mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza katika michuano ya wazi ya Us Open. Watson amepoteza mchezo huo mbele ya Mmarekani Lauren Davis kwa seti 7-6 (7-3) 7-6 (7-0). Nyota huyu ambaye ali… Read More

0 comments:

Post a Comment