Friday, September 11, 2015

KUELEKEA MAN UNITED VS LIVERPOOL : TETESI ZINASEMA KWAMBA DE GEA ANAWEZA KUANZA MECHI HII

gera

Jana nikiwa hapa Manchester alionekana wakala wa De Gea ambapo baada ya mazoezi inasemakana kulikua na kikao kati ya Van Gaal na De Gea ili kumaliza tofauti zao. Sasa kutokana na sababu za Van Gaal kwanini alikua hampangi kwenye mechi De Gea, alisema kwamba mchezaji huyo hayupo focus kutokana na mambo ya uhamisho wake yanavyoendelea.
Sasa hivi mambo hayo yameisha na inaaminika kwamba wamekaa na kumaliza tofauti kati yao. Pia kizuri zaidi wanategemea kusaini mkataba mpya wa De Gea kuendelea kukaa ndani ya Man united.
Sasa tetesi mpya zinasema kwamba mchezaji huyo bora wa Manchester united kwa msimu wa 2014/15 ataanza kwenye kikosi cha mechi dhidi ya Liverpool. Kutokana na tofauti kuisha na mambo ya uhamisho kupita hivi sasa kila mtu anategemea kumuona De Gea akicheza tena.

SHUDATE BLOG

0 comments:

Post a Comment